Friday, February 15, 2013

Anna Michael utakumbukwa daima kwenye Movie bongo, Tanzania




                                            Marehemu Anna Michael enzi ya uhai wake                                 
Jina kama Sina alilotambanalo katika kikundi cha Kidedea au Tunu alilovuma nalo katika sinema ya I love you,ni kilelezo tosha  kama uwezo wa Anna Michael katika sanaa ya kuigiza ulikuwa wa kiwango cha juu.

Majina hayo yalitaka kufuta jina lake halisi la Anna Michael, alilopewa na wazazi wake. Wahenga walisema kila kilichokuwa kizuri hakidumu sana, ni kauli inayowakilisha ukweli wa machungu yanayouma. Lakini yote ni mipango ya mwenyezi mungu.

Licha ya wazazi wake, mtoto wake, ndugu, marafiki, waigizaji wenzake, wapenzi na mashabiki wake walimpenda, lakini mungu alimpenda zaidi na kumchukua.

Ni miaka minne sasa tangu Anna Michael hatutoke kimwili na kiroho lakini kazi zake zitaendelea kuwepo katika maisha yetu ya kila siku.

Kila utakapotazama sinema ya Uwanja wa dhambi, I love you, Picnic na Confess. Utaweza kujionea kipaji alichobahatika kuwa nacho marehemu.

Wasanii wanaochipukia wangetafuta sinema alizocheza waweze kujifunza mambo muhimu.

Marehemu alikuwa anavaa taswira anayotakiwa kucheza, ni vigumu kwa sasa kupata wasanii wenye uwezo huo. Wengi wanapoteza uhalisi wanapoigiza.

Kuna wale wanaopoteza uhalisi wa sauti, muonekana na hata mavazi. Kazi kwenu wasanii chipukizi. 

No comments:

Post a Comment