Monday, February 11, 2013

Mavazi yanayotumika yanaondoa uhalisi wa sinema Tanzania



Imebainika kama watazamaji wengi wa sinema hasa wabongo wanavutiwa na mavazi ya waigizaji. Uchunguzi uliofanywa umefanikiwa kugundua kama watazamaji wa kiume wanavutiwa zaidi ya mavazi ya waigizaji wa kike, hasa wanapokuwa katika scene inayowaonyesha wamevaa night dress.

Wanaume wengi wanadai night dress zinawapendeza wanawake, Zinawachochea na kuamsha hisia zilizolala. Mavazi mengine yanayowavutia ni vimi, yaani vile vimini vifupi sana kuvuka magoti, Sambamba na zile nguo za kubana zinazoonyesha shepu zao.

Wanaume wengine wanavutiwa na aina ya viatu wanavyovaa waigizaji wa kike, wengi wanapenda kumuona muigizaji amevaa viatu virefu kama vile 6inch stiletto high heels, high heels Pumps, high heels Platform, Wedge heels, Metal Spike high heels, Boots high heels and high heels Sandals.

Kwa upande wa wanawake wanavutika na mitindo wanayovaa waigizaji wa kike, wapo wanaongalia mitindo ya nguo, nywele na viatu. Wengine wanakwenda mbali sana na kujikuta wakivutiwa na aina ya uongeaji na hata mapozi ya msanii.

Kwa kuzingatia hilo, ndiyo maana sinema nyingi za kibongo zinapoteza uhalisi kwa ajili ya kutaka kuwafurahisha wapenzi wao.

Utakuta msichana anacheza nafasi ya kijijini, amevaa mavazi ya kimjini. Au msichana anacheza kama sekretari amevaa kimini. Au msichana anaonekana yupo nyumbani amevaa kiatu kirefu. Kwa ufupi uhalisi wa sinema za kitanzania unapotea kwa kuendekeza ujinga.


No comments:

Post a Comment