Saturday, February 16, 2013

Alwatan yawakumbuka waliotangulia mbele ya haki




Kikundi cha Alwatan Artist Theater chenye makao yake makuu Ilala Kimako, kimefanikiwa kutayarisha sinema nane, miongoni mwa sinema hizo ni pamoja na Uwanja wa dhambi, Popobawa, I love you, Picnic, Bunge la wachawi, Zindiko, Confess na Julio na Romeo inayotarajiwa kuingia mtaani hivi karibuni.

Kwa mujibu wa msemaji wa kikundi hicho, Belinda amesema kikundi kimeondokewa na wasanii wake tegemezi kama Anna Michael, Nyanda Nduta, Zainabu Mbavumbili aliyejitenga na kujiunga na kikundi kinachitwa Kitisa kabla ya kufikwa na umauti.

Mwingine aliyefariki ni mwandishi wa script, muigizaji na Director, Salum Karanda. Licha ya kufanya makubwa katika sanaa ya sinema, lakini vifo vya wasanii hao havikupata nafasi kubwa  katika vyombo vya habari.

Kwa mfano Salum Karanda aliyetayarisha sinema nyingi sana, pia alikuwa akiandika habari katika magazeti ya kila wiki kama mwandishi wa kujitegemea.

Miongoni mwa sinema alizoshiriki kama muongozaji msaidizi ni Mzee wa Busara, Siri, Shetani wa mahaba, Roho mbili, Jinamizi, Kisu, Bosi, Best friend, Uwanja wa dhambi, I love you na Picnic na nyingine. Alizoshiriki kama muongozaji mkuu ni Fadhila, Mama Mwenye Nyumba, Gauni la Marehemu, Hofu na nyingine nyingi

No comments:

Post a Comment