Mtunzi kitabu cha Ngoswe, Edwin Semzaba akiwa na rafiki yake mwenye miwani
Unaweza kushangaa kusikia hivyo, ila vipo vitabu vilivyotengenezwa sinema, miongoni mwa vitabu hivyo ni MAMBO YA NGOSWE kilichotungwa na Edwin Semzaba , kimechapishwa mwaka 1996 na Dar es Salaam University Press.
Kitabu hicho kilitayarishwa kuwa sinema na kampuni ya utayarishaji sinema Tanzania, hata hivyo haikuweza kutoka kwa wakati huo mpaka mwaka 2005. Ilipochukuliwa na kampuni ya Heko Production na kuikarabati kwa kuiongezea ubora na hatimaye kuisambaza madukani.
Kabla ya kitabu hicho kutayarishwa sinema, kiliwahi kutumika katika mchezo wa redio. Uliorushwa hewani na redio Tanzania hivi sasa ni TBC Redio.
Kitabu kingine kilichotengenezwa sinema na NGOME YA NG’WANAMALUNDI kilichotungwa na Emmanuel Mbogo, kilitayarishwa sinema na kampuni ya Heko Production mwaka 2005. Director akiwa marehemu Hammie Rajabu, Executive Producer akiwa marehemu Ben R Mtobwa, Production Manager akiwa Haji Dilunga.
Kitabu cha LAZIMA UFE JORAM kilitengenezwa sinema, kitabu hicho kilitungwa na Marehemu Ben R Mtobwa, kilichapishwa na kampuni ya Heko Publishers mwaka 1985, kilitayarishwa sinema na Heko Production mwaka 2006.
Director wa sinema hiyo alikuwa Bob Masha, Script writer alikuwa Haji Dilunga, Executive Producer Marehemu Ben R Mtobwa, Production Manager alikuwa Ngabwe.
SIMU YA KIFO ni kitabu kingine kilichotengenezwa sinema, kitabu hicho kilitungwa na Faraji Katarambula. Marehemu Hammie Rajabu aliandika Script na ndiye aliyekuwa Director wa movie hiyo.
Kitabu kingine ni MZEE WA BUSARA kilichotungwa na Sultan Tamba, script aliandika mwenye sambamba na kuidirect mwenyewe akisaidiwa na Marehemu Salum Karanda.
No comments:
Post a Comment