Showing posts with label Kitanzania. Show all posts
Showing posts with label Kitanzania. Show all posts

Saturday, November 29, 2014

Sinema kumi za kitanzania zinazofanya vizuri sokoni

Mwaka huu kuanzia Januari mpaka Novemba zimeingia sokoni sinema nyingi sana,  kila sinema ilikuwa na utamu sambamba ubora wake, watayarishaji na waigizaji sambamba waongozaji walijitahidi kila mmoja kuhakikisha anafanya kazi nzuri itakayokubalika na jamii.
Kama tulivyosema mwanzo sokoni zimeingia sinema nyingi,  kati ya hizo  sinema kumi zimetokea kupendwa na watu wengi sana.  Tafiti za kupendwa  kwa sinema hizo zilizofanyika katika mkoa wa Dar es Salaam  na Arusha kwa wauzaji wa maduka ya jumla na  maduka ya rejareja,  sambamba na wauzaji wanaotembeza mitaani maarufu kwa jina la wamachinga.

 1.                                                       Jamila na pete ya ajabu
                                      Jamila imetokea kuvuwatia watoto wengi sana kwa mujibu wa
                                                   wadau wetu   waliotupatia taarifa hizo
                                                                   

                                                                                                                                                      
 2                                                                       Chausiku   

Chausiku imetokea kuwa gumzo kubwa katioka maeno ya uswahili
3                                                                Siri ya Giningi
                                                                             

                                                                                   
 4                                                             Zena na Betina
                                                                          
5                                                              Hakumu ya ndoa yangu
                                                                             
6                                                               Tom Boy  
                                                                       


 7                                                        Uliyemchokoza kaja
                                                                           



 

8                                                                    Nahama

                                                                           

 9                               Nendeze Mwali wa Kizaramo ( Sinema hii haina kava)

                                                                         

10                                                         Kwanini Mama 
                                                                        

                                                                     



Saturday, February 16, 2013

Movie Kitanzania bila mastaa haziuziki?


Baadhi ya wasambazaji wa sinema  nchini,  wameibuka na  kituko kitakachosambaratisha soko la sinema za kibongo, kama  hawatakubali kuachana  na mawazo yao mgando ya kudai sinema bila ya msanii maarufu huwezi kuuza.

Uchunguzi  wetu umeonyesha  kabla ya kuwa na wasanii maarufu, watanzania walikuwa  wakinunua sinema na kuangalia,  wapo waliokuwa wakinunua sinema za kihindi bila ya kuwafahamu waigizaji hao kama maarufu au sio maarufu.

Wapo waliokuwa wakinunua sinema za kichina, kijapan na kizungu. Baada ya kuingia sinema za kinaigeria watanzania walizinunua,  walipokuwa wananunua hawakujua kama wasanii hao ni maarufu, ila walinunua kwa ajili ya kupata burudani ya sinema.

Kama wasambazaji wa nchi nyingine wangekuwa na mawazao kama ya wasambazaji wetu. Tusingeshuhudia  waigizaji wapya wakiibuka kila kukicha. Tungeendelea kushuhudia wale wale wa zamani ambao umri umeanza kuwatupa mkono. 

Wasambazaji wanatakiwa kufahamu kama waigizaji wanaitwa mastaa hivi sasa, kuna watu wamewafikisha hapo,  hawakuzaliwa wakiwa mastaa. Mnatakiwa na nyinyi kuzalisha wapya sio kutafuta mastaa walitengenezwa na wenzenu.


Unafahamu vitabu vya kitanzania vilivyotengenezwa sinema


Mtunzi kitabu cha Ngoswe, Edwin Semzaba akiwa na rafiki yake mwenye miwani
 
Unaweza kushangaa kusikia hivyo, ila vipo vitabu  vilivyotengenezwa  sinema,  miongoni mwa vitabu hivyo ni  MAMBO YA  NGOSWE  kilichotungwa  na Edwin Semzaba , kimechapishwa  mwaka  1996  na Dar es Salaam University Press.

Kitabu  hicho  kilitayarishwa  kuwa sinema  na kampuni ya utayarishaji sinema  Tanzania, hata hivyo haikuweza kutoka kwa wakati huo mpaka  mwaka 2005. Ilipochukuliwa na kampuni ya Heko Production  na kuikarabati  kwa kuiongezea ubora na hatimaye kuisambaza madukani.

Kabla ya kitabu hicho kutayarishwa  sinema,  kiliwahi kutumika katika mchezo wa redio. Uliorushwa hewani na redio Tanzania  hivi sasa ni TBC Redio.

Kitabu kingine kilichotengenezwa  sinema  na  NGOME  YA   NG’WANAMALUNDI  kilichotungwa na Emmanuel Mbogo, kilitayarishwa sinema na kampuni ya Heko Production mwaka 2005.  Director  akiwa  marehemu Hammie Rajabu, Executive Producer  akiwa marehemu Ben R Mtobwa, Production Manager akiwa Haji Dilunga.

Kitabu cha   LAZIMA UFE JORAM  kilitengenezwa sinema, kitabu hicho kilitungwa na Marehemu Ben R Mtobwa,  kilichapishwa na  kampuni ya  Heko Publishers mwaka 1985,  kilitayarishwa  sinema  na  Heko Production mwaka 2006.

Director wa sinema hiyo alikuwa Bob Masha,  Script writer alikuwa Haji Dilunga, Executive Producer Marehemu Ben R Mtobwa, Production Manager  alikuwa  Ngabwe.

SIMU YA KIFO ni kitabu kingine kilichotengenezwa sinema, kitabu hicho kilitungwa na Faraji Katarambula. Marehemu Hammie Rajabu  aliandika Script  na ndiye aliyekuwa Director wa movie hiyo.

Kitabu kingine ni MZEE WA BUSARA kilichotungwa na Sultan Tamba,  script  aliandika mwenye sambamba na kuidirect  mwenyewe  akisaidiwa na Marehemu Salum Karanda.