Saturday, February 16, 2013

Movie Kitanzania bila mastaa haziuziki?


Baadhi ya wasambazaji wa sinema  nchini,  wameibuka na  kituko kitakachosambaratisha soko la sinema za kibongo, kama  hawatakubali kuachana  na mawazo yao mgando ya kudai sinema bila ya msanii maarufu huwezi kuuza.

Uchunguzi  wetu umeonyesha  kabla ya kuwa na wasanii maarufu, watanzania walikuwa  wakinunua sinema na kuangalia,  wapo waliokuwa wakinunua sinema za kihindi bila ya kuwafahamu waigizaji hao kama maarufu au sio maarufu.

Wapo waliokuwa wakinunua sinema za kichina, kijapan na kizungu. Baada ya kuingia sinema za kinaigeria watanzania walizinunua,  walipokuwa wananunua hawakujua kama wasanii hao ni maarufu, ila walinunua kwa ajili ya kupata burudani ya sinema.

Kama wasambazaji wa nchi nyingine wangekuwa na mawazao kama ya wasambazaji wetu. Tusingeshuhudia  waigizaji wapya wakiibuka kila kukicha. Tungeendelea kushuhudia wale wale wa zamani ambao umri umeanza kuwatupa mkono. 

Wasambazaji wanatakiwa kufahamu kama waigizaji wanaitwa mastaa hivi sasa, kuna watu wamewafikisha hapo,  hawakuzaliwa wakiwa mastaa. Mnatakiwa na nyinyi kuzalisha wapya sio kutafuta mastaa walitengenezwa na wenzenu.


No comments:

Post a Comment