Tuesday, February 19, 2013

Sinema kimataifa, Kambi kuigiza Ghana na Van Vicker


Hashim Kambi
                                      Van Vicker

Muigizaji wa filamu nchini Hashimu Kambi amefungua mwaka huu kwa neema ambapo hivi sasa muigizaji huyo anatarajia kusafiri kuelekea nchini Ghana na Nigeria kwa ajili ya kufanya kazi akiwa ni muigizaji mkuu msaidizi.

Kwa mujibu Televisheni ya EATV, Hashimu amesema kuwa amepata mwaliko huo baada ya kazi zake kumfikia msanii ambaye ni muongozaji wa filamu mahiri katika nchi ya Nigeria anayejulikana kwa jina la Van Vicker.

Aidha akiwa nchini Nigeria na Ghana Hashimu anatarajia kushiriki katika filamu inayoitwa Day after Death itakayofanyika kwa muda wa siku saba jijini Accra na siku saba kwenye jiji la Lagos, ambapo inamuweka katika nafasi nzuri ya ushiriki wake filamu za kimataifa baada ya marehemu Steven Kanumba aliyeweza kuipeperusha vyema bendera ya taifa kimataifa.

No comments:

Post a Comment