Monday, February 11, 2013

Sinema Tanzania, muonyesha video anavutika na bodi ya Halima

 
                                                                 Halima Madiwa pozi

Hebu jaribu kusikia kihoja cha mdau huyu wa muvi, anayeitwa  Danny Alex  anayemiliki banda la video maeneo ya  Kipawa. Amesema  miongoni mwa waigizaji wanaomvutia ni Halima Madiwa.

Amedai alianza kuvutiwa na umbo la Halima Baada ya kuona picha yake kwenye gazeti la udaku.

Alex amesema picha hiyo ilikuwa na maelezo yanayosema wanaume wanamsumbua kutokana na makalio yake kuwa makubwa.

Kunzia siku hiyo akaanza kufuatilia sinema alizocheza Halima kwa bahati nzuri alibahatika kupata sinema ya Sound of Death. Katika movie hiyo hakuweza kumuona vizuri kwa sababu alicheza kipande kidogo sana. Hata hivyo alicheza akiwa amekaa.

Sinema nyingine aliyocheza ilikuwa Secret file, pia alicheza kama msichana wa mapokezi akiwa amekaa. Kwenye sinema ya Devil Kingdom amecheza kama sekretari, alionekana akimpa barua Marehemu Kanumba.

Alifanikiwa kuona bodi yake ila alichezeshwa kipande kidogo. Swali lake kwa watayarishaji, anataka kujua vigezo gani vinavyotumika kumpatia nafasi kubwa ya kuigiza msanii. Kama ni umbo na uzuri, mbona Halima analipa kuliko waigizaji wengine.

No comments:

Post a Comment