Showing posts with label Tanzania. Show all posts
Showing posts with label Tanzania. Show all posts

Monday, February 2, 2015

Waigizaji wa kiume kumi wa Tanzania wenye mvuto kwa mashabiki

Waigizaji wa kiume kumi wa Tanzania wenye mvuto kwa  wapenzi na mashabiki wanaotazama sinema za kibongo,  listi hiyo tumeipata kutokana na kuongea na waonyeshaji wa video katika mabanda ya video.  Wakodishaji wa DVD katika maduka ya kukodisha ya jijini Dar es salaam hasa maeneo ya uswahilini kunakotizamwa sana sinema za kibongo, maduka hayo ni maarufu kama maktaba za uswahilini au uswazi.  Fuatilia listi ya mwigizaji namba moja mpaka kumi.  Muhimu kuzingatia ni listi ya blog yetu, sio mawazo ya watazamani wa nchi yote.                                                          
1. Salim Ahmed aka Gabo

                                                    
                                                                  2. King Majuto 
                                                                3. Haji Adam                                                                                                                                       
                                                                   4. Jacob Stephen aka JB
                                                                  5.Lucas Lazaro Mhuvile .ak.a Joti
                                                                          
                                                                 6. Rammy Galis
                                                               
                                                           7.  Hissani Muya  a.k.a Tino
                                                                      
                                                                 8. Abdul Mohamed a.k.a Ben Branco
                                                                                 

                                                                 9. Haji Mboto
                                                                              
                                                                  10.Musa Kitale





     

Sunday, February 1, 2015

Waigizaji wa kike kumi wa Tanzania wenye mvuto kwa mashabiki

Waigizaji wa kike kumi wa Tanzania wenye mvuto kwa  wapenzi na mashabiki wanaotazama sinema za kibongo,  listi hiyo tumeipata kutokana na kuongea na waonyeshaji wa video katika mabanda ya video.  Wakodishaji wa DVD katika maduka ya kukodisha ya jijini Dar es salaam hasa maeneo ya uswahilini kunakotizamwa sana sinema za kibongo, maduka hayo ni maarufu kama maktaba.  Fuatilia listi ya mwigizaji namba moja mpaka kumi.  Muhimu kuzingatia ni listi ya blog yetu, sio mawazo ya watazamani wa nchi yote.                                                          
Riama Ally

                                                                1. Riama Ally


                                                                  2. Shamsa Ford
                                                                                                                           
                                                                               Salma Jabu
                                                                3. Salma Jabu                                                                                                                                       
                                                                      Irene Paul
                                                                   4. Irene Paul

                                                                           
                                                                      Cathy Rupia
                                                                  5.Cathy Rupia
                                                                          
                                                                      Wellu Sengo

                                                               6. Wellu Sengo
                                                               
                                                               Elizabeth Chijumba
                                                                                  
                                                              7.Elizabeth Chijumba
                                                                      
                                                                   Hamisa Mabeto

                                                                      8. Hamisa Mabeto 
                                                                                 

                                                                 9. Jennifer Kyaka
                                                                              
                                                                         Flora Mvungi
                                                                  10. Flora Mvungi





     

Thursday, July 18, 2013

Danny Schechter ameitangaza Tanzania kwenye Movie ya Mandela

                                                                              
                                                                     Danny Schechter
Danny Schechter  a.k.a The News Dissector kwa wale wasio mfahamu ni mtayarishaji  kama sio mtengenezaji wa sinema ya Nelson Mandela – “Countdown to Freedom” na “Mandela in America” ametaka dunia kuiheshimu Tanzania kwa nafasi yake kubwa kwenye kutengeneza demokrasia Afrika Kusini.
Schechter anayefanya dokumentari ya utengenezaji wa filamu ya Long Walk to Freedom kama alivyotakiwa na Nelson Mandela mwenyewe, alisema Tanzania ilitoa ushirikiano mkubwa kukomboa mataifa mengi ya Afrika ikiwemo Afrika Kusini.
Jumapili katika Tamasha la ZIFF ilikuwa ni siku ya kuangalia Afrika Kusini kabla na baada ya Uhuru. ZIFF iliweka siku maalumu ya Afrika Kusini kutokana na maendeleo ya hali ya afya ya Nelson Mandela ambayo sasa inazungumzwa duniani kote.
Mandela ambaye katika dokumentari hiyo anaonekana akifafanua vitu mbalimbali, alielezwa na Schechter kama mtu maarufu ambaye hakutaka kuitwa mtakatifu pamoja na kwamba aliombwa kutengenezewa sanamu na kuwataka wasifanye hivyo na badala yake kusaidia ujenzi wa zahanati.
Alisema dunia inapaswa kutambua kwamba katika ukombozi wa Afrika Kusini, Tanzania ni nchi muhimu ingawa dunia inaonekana kutotambua hilo lakini wenyewe wa Afrika Kusini wanafahamu.
Alisema baada ya kuwapo na nia ya kutengeneza filamu yake, Madiba alimwandikia barua ya kumtaka kutengeneza dokumentari inayohusu utengenezaji huo kwa kuhakikisha ukweli uliopo kama unazingatiwa.
Alisema hali hiyo ilimfanya kufika Tanzania japo alishawahi kufika wakati wa harakati za ukombozi. Schechte ambaye ni mwandishi wa habari za uchunguzi, mtengeneza sinema huru, bloga na mhakiki vyombo vya habari, alisema ni vyema dunia ikatambua mchango wa Tanzania kwa ukombozi si wa Afrika Kusini, bali na mataifa mengine ya Afrika.
Alisema pamoja na utawala wa Makaburu kuzishambulia nchi zilizokuwa zinasaidia ANC kama Zimbabwe, Msumbiji, Angola na Zambia, ilishindwa kufanya hivyo kwa Tanzania ambayo licha ya kuwa na makambi ya mazoezi ya kivita, pia ilikuwa na shule za kufunza viongozi wa baadaye wa Afrika Kusini, Morogoro.
Dukumentari hiyo yenye tofauti kubwa na zile zinaozotengenezwa kwa ajili ya kuoneshwa katika televisheni, inamweleza Mandela kama mtu wa watu huku waliohojiwa wakielezea matumaini na nini kinafanyika.

Friday, March 29, 2013

Unamfahamu Angelina Jolie wa Tanzania

Angelina Joel mwenyewe wa Majuu Kama humjui Angelina Jolie wa Tanzania, kuanzia sasa unatakiwa kumfahamu kuwa ni Irene Paul. Mwigizaji anayekuja juu sana katika ulimwengu wa sinema za kibongo. Udhibitisho kama anakuja katika uigizaji. Unaweza kumwangalia katika sinema ya The Morning Alarm aliyocheza na Marehemu Steven Kanumba na Abdul Ahmed maarufu kama Ben. Stori imetungwa na Mtitu G Game. Script imeandikwa waandishi wa wawili, Haji Dilunga na Ally Yakuti. Baada ya kushiriki kucheza sinema za watu, hivi sasa Irene Paul ametayarisha sinema yake mwenyewe inayoitwa Kalunde. Ukipata DVD yake unaweza kumshuhudia Angelina Jolie wa bongo. Iren Paul a.k.a Angelina Joel wa bongo

Tuesday, February 19, 2013

Sinema Tanzania, Mchungaji bado anamwandama Kanumba

                                              Steven Kanumba         
Kitendo cha baadhi ya wananchi kutumia jina la msanii aliyefariki kujipatia kipato au umaarufu ni kitu kibaya, kinachotakiwa kupigwa marufuku na kuwakamata wahusika na kufikisha mbele ya vyombo vya sheria.

Swahili Cinema News imeshuhudia mtu anayejiita Mchungaji George Kairuki akitumia jina la Marehemu Steven Kanumba kujipatia umaarufu katika kiwanja kilichokuwa Buguruni chama karibu na shule ya msingi, pamoja na kituo cha basi.

Mchungaji huyo aliibuka mara baada ya kifo cha Marehemu Kanumba na kueleza kama marehemu alikuwa muumini wa Freemasons, madai ambayo hakuna aliyekuwa na uhakika nayo.

Hata hivyo, kwa akili za kawaida madai hayo kwa sasa hayana umuhimu wowote, hakuna aliyetaka kufahamu kama alikuwa muumuni wa Freemasons. Kwa sababu haisaidi chochote hata watu wakifahamu.

Kikubwa anachofanya mchungaji huyo ni kujitafutia umaarufu kupitia mgongo wa marehemu Kanumba, taarifa ambazo kwa upande mwingine zilionyesha kumjenga kwa kumpatia umaarufu ili watu wajiunge na kanisa lake.
Kama lengo ni kutoa taarifa za Kanumba kujiunga na Freemasons, alikwishatoa baada ya kifo chake, vyombo vya habari viliandika na kutangaza.

Kwa hiyo hakuwa na sababu ya kuendelea kueleza taarifa hizo kwenye viwanja vya wazi. Ukifuatilia matukio ya mchungaji huyo, utagundua anachofanya ni kujitafutia umaarufu, mwaka jana alijisingizia kifo kilichofanana na kifo cha Marehemu Kanumba, magazeti ya udaku yaliandika taarifa zake na kuonyesha picha aliyokuwa kwenye jeneza.

Baada ya muda mfupi aliibuka kiwanja cha Buguruni akitoa maelezo ya namna Kanumba alivyokufa. Mchungaji huyu ni hatari anayestahili kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Wadua, Shirikisho, Familia na marafiki wa marehemu jitokeni kumtia adabu mtu huyo anayeendelea kujipatia umaarufu sambamba na kipato kupitia jina la Kanumba. Kwani hawezi kuzungumzia Freemasons bila ya kutaja jina la marehemu Kanumba.

Ikiwa nia yake ni safi, angeelezea imani ya Freemasons kwa kumtaja aliyekuwa kiongozi wa Afrika Mashariki, Sir Andy Chande , sio vizuri kumtaja mtu aliyekufa ambaye hawezi kujitetea.

Kwa mujibu wa maelezo yake anadai alikuwa anajua kama Kanumba ni muumini wa Freemasons kabla ya hajafa. Kama ni kweli, kwanini alikaa kimya mpaka alivyokufa na kuibuka kuanza kuzungumza mambo ambayo hayana faida kwa jamii. Badala yake ni kuhamasisha jamii ya vijana kutaka kujiunga na imani. Sisi wana Swahili Cinema News tunasikitishwa na tabia ya mchungaji huyo.

Movie Tanzania, Inawezekana kila mwigizaji kutayarisha sinema?

  Inawezekana kila mwigizaji kuwa mtayarishaji wa sinema. Jibu linaweza kuwa ndio au hapana, kwa sababu utayarishaji wa sinema unaweza kufanywa na mdau yoyote mwenye uwezo wa fedha, ila awe anajua sanaa ya sinema kwa undani zaidi. Vinginevyo anaweza kuingia mikononi mwa wababaishaji na kujikuta akipoteza muda na fedha.

Mwigizaji anaweza kutayarisha sinema ila ni lazima awe na upeo mkubwa wa kutayarisha sio kuigiza, unaweza kuwa mwigizaji mzuri lakini ukashindwa kuwa mtayarishaji au muongozaji mzuri yaani director mzuri.

Wapo madirector wazuri sana, lakini hawawezi kuigiza. Kwa sababu hawana taranta au tunaweza kuita kipaji, wapo waandishi wazuri wa hadithi na vitabu, lakini hawawezi kuandika script.

Wapo wachezaji wazuri wa soka lakini hawezi kuwa makocha wazuri, wapo makocha wazuri lakini hawakuwahi kucheza mpira kwa kiwango cha kuitwa mastaa. Kwa hiyo ni vizuri kujikagua kama una taranta kabla ya kufanya chochote unachotaka kufanya.

Wapo waigizaji wenye taranta ya kutayarisha sinema na kuziongoza vizuri, mfano mwigizaji Mel Colm Cille Gerard Gibson wa Marekani, wengi wanamfahamu kwa Mel Gibson ni mwigizaji, mtayarishaji, mwandishi wa script na muongozaji. Moja ya sinema aliyoongoza ni Apocalypto

Marekani na Ulaya wapo wengi wenye uwezo wa kufanya yote katika utengenezaji wa sinema, pia wapo ambao hawawezi. Wanatoa nafasi kwa wenzao wanaoweza.
Kwa Tanzania hali ni tofauti, wengi hawawezi kutayarisha sinema wala kuziongoza. Ila wanajilazimisha kufanya hivyo kwa sababu wanajiona mastaa, ukweli unabaki kama sinema wanazotayarisha zinakuwa hazina ubora unaotakiwa.

Ukijiona huna uwezo wa kuandika script, kutayarisha na kuongoza. Tafuta wadau wenye uwezo wa kufanya kazi hizo kwa ajili ya kupata sinema nzuri. Matokeo ya kila kitu kutaka kufanya mwenyewe ni kutayarisha kazi mbovu.

Aliyekupa fedha za kutayarisha sinema akigundua sinema yako haipendwi na watazamaji, atakumwaga na hatimaye kupotea katika soko la sinema kabisa.

Kama lengo la wadau ni kuendeleza sekta ya uigizaji, waigizaji wanaopata bahati ya kuingia mikataba na wasambazaji kwa ajili ya kutayarisha sinema, wasiwe wabinafsi. Kuendekeza ubinafsi ni kuua sekta sinema, inayoongoza hivi sasa kwa kutoa ajira kwa vijana na wazee.
 
 
 
 

Saturday, February 16, 2013

Camera man, mwigizaji wanapokuwa madirector



                                                                   Camera man
Imekuwa kawaida katika nchi yetu ya Tanzania kumsikia  camera man au mwigizaji akibishana na Director.  Ugonjwa huu usipokemewa unaweza kuambukiza kizazi kijacho katika sanaa ya sinema.

Kitaalamu  production yote ipo chini ya director,  yeye  ndiye mwenye maamuzi ya mwisho. Anapoamua  jambo lolote hakuna mwenye ubavu wa kubisha, mliokuwa hapo mnaweza kumpa ushauri,  ni maamuzi yake kukubali au kukataa.

Mfano mzuri  director ni kocha wa timu ya mpira,  huwezi kuingilia maamuzi ya kochi katika kutayarisha kikosi chake.

Kwa upande wa utayarishaji wa sinema  madirector wanaingilia katika kufanya maamuzi yao,  matokeo yake wanajikuta wanatayarisha sinema  yenye makosa. 

Makosa yenye yanasababishwa na kutokuwa makini. Mwigizaji anambishia director, camera man anambishia director anajifanya anajua sana,  matokeo ya mabishana hayo ni Director kupoteza umakini na kufanya kazi mbovu.

Camera man  na waigizaji  tuwaache  madirector wafanye kazi zao,  kuwaingilia kuna sababisha kuendelea kushuhudia sinema zenye mapungufu na makosa ya kijinga, ambayo hayahitaji  elimu ya chuo kikuu kuweza kuyabaini.

Kama wewe mwigizaji fanye kile ulichokufikisha pale, mambo ya kuelekeza hayakuhusu. Nawe camera man fanye kazi yako ya kupiga picha, kuelekeza waigizaji namna ya kucheza sio kazi yako. Hiyo ni kazi ya Director na msaidizi wake.

Kila mmoja akizingatia jukumu lake, makosa ya kipumbavu katika sinema zetu yatapungua.  Ushauri kwenu wenye tabia hizo, kusema  ACTION   na CUT sio sababu ya kujiona unaweza kudirect movie.

Kuidirect movie ni zaidi ya ACTION  na CUT,  tuwape nafasi  madirector kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi. Unajua kama kusimama nyuma ya camera sio sababu ya kuitwa camera man, au kubeba  jezi na mpira sio kigezo cha kuitwa mchezaji. Au kubeba gitaa sio sababu ya kuitwa mwanamuziki. Au kushinda kutwa chumba cha habari huwezi kuitwa mwandishi au mtangazaji. Unaweza kuwa mfagiaji.

Bongo movie, Sound of Death inaoongoza kwa mastaa wengi Tanzania


                                                         Tumaini Bigirimana
                         Jacob Steven
                         Patcho Mwamba
                                                            Hemed Suleiman
                                                        Auntie Ezekiel
                      Yusufu Mlela
Sinema iliyotungwa na kuandikwa script na Haji Dilunga kisha kuongozwa na Mtitu G Game, inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya waigizaji maarufu hapa nchini.

Swahili Cinema News ilishuhudia mabishano makali ya wapenzi na mashabiki ya sinema za kibongo katika kibanda cha video.

Mabishano hayo yalidai Sound of Death ni sinema pekee iliyokusanya waigizaji wengi wenye majina makubwa hapa bongo.

Miongoni mwa majina ya waigizaji walioshiriki katika movie hiyo ya aina yake ni pamoja na Auntie Ezekiel, Jacob Steven, Rose Ndauka, Hemedi Suleiman, Flora Mvungi, Yusuf Mlela, Tumaini Bigirimana, Patcho Mwamba, Mayasa Mrisho.

Wengine ni Hidaya Njaidi, Tito, Masinde, Grace Mapunda, Mariam Georger, Abdul Ahmed a.k.a Ben, Bakari Makuka, Maua na wengine

Mpaka mwanahabari anaondoka hapo hakuna mshindi wa mabishano hayo, ila utafiti wetu umefanikiwa kugundua kwamba Sound of Death inaweza kuwa miongoni mwa sinema iliyokusanya idadi kubwa ya waigizaji wenye majina makubwa kwa mwaka 2012.

Friday, February 15, 2013

Anna Michael utakumbukwa daima kwenye Movie bongo, Tanzania




                                            Marehemu Anna Michael enzi ya uhai wake                                 
Jina kama Sina alilotambanalo katika kikundi cha Kidedea au Tunu alilovuma nalo katika sinema ya I love you,ni kilelezo tosha  kama uwezo wa Anna Michael katika sanaa ya kuigiza ulikuwa wa kiwango cha juu.

Majina hayo yalitaka kufuta jina lake halisi la Anna Michael, alilopewa na wazazi wake. Wahenga walisema kila kilichokuwa kizuri hakidumu sana, ni kauli inayowakilisha ukweli wa machungu yanayouma. Lakini yote ni mipango ya mwenyezi mungu.

Licha ya wazazi wake, mtoto wake, ndugu, marafiki, waigizaji wenzake, wapenzi na mashabiki wake walimpenda, lakini mungu alimpenda zaidi na kumchukua.

Ni miaka minne sasa tangu Anna Michael hatutoke kimwili na kiroho lakini kazi zake zitaendelea kuwepo katika maisha yetu ya kila siku.

Kila utakapotazama sinema ya Uwanja wa dhambi, I love you, Picnic na Confess. Utaweza kujionea kipaji alichobahatika kuwa nacho marehemu.

Wasanii wanaochipukia wangetafuta sinema alizocheza waweze kujifunza mambo muhimu.

Marehemu alikuwa anavaa taswira anayotakiwa kucheza, ni vigumu kwa sasa kupata wasanii wenye uwezo huo. Wengi wanapoteza uhalisi wanapoigiza.

Kuna wale wanaopoteza uhalisi wa sauti, muonekana na hata mavazi. Kazi kwenu wasanii chipukizi.