Showing posts with label mastaa. Show all posts
Showing posts with label mastaa. Show all posts
Sunday, March 1, 2015
Viatu vya kishetani, ukivaa unamsambaza kwa nguvu moja.
Ukivaa unaendelea kumtukuza na kumsambaza shetani kwa wengi, sio kila kinachotengenezwa na wabunifu ni lazima ukivae. Vitu vingine vinatengenezwa kwa sababu maalumu, watengenezaji wanajua wanachofanya, hakuna anayebahatisha katika hilo. Miongoni mwa wabunifu na watengenezaji wa mitindo mbali mbali ni wafuasi wa dini ya shetani. Kuweni makini katika kuchagua aina gani ya kiatu unachotaka kuvaa. Hasa kina dada wanaongoza kwa kuwa na mitindo mingi ya viatu na nguo. Kwa vile wabunifu wanajua kama waigizaji, wanamuziki na wanamitindo wa mavazi ni watu wanaotazamwa sana na jamii, wanawavisha viatu hivyo kwa lengo la kuvitafutia soko na umaarufu miongoni mwa jamii ili shetani aweze kuwa na nguvu. Hivi sasa viatu hivyo vimeanza kutumika sana katika sinema mbali mbali au katika baadhi ya video za wanamuziki maarufu. Wakati mwingine vimekuwa vikitumika katika majukwaa ya wanamitindo. lengo ni kusambaza nguvu za shetani. kuwa makini kama unapenda kuigi kila kitu.
Wednesday, January 28, 2015
Mastaa wengi wanakichaa cha kuvaa nusu uchi
Watu wengi maarufu kama vile waigizaji wa sinema na wanamuziki wanaongoza kuwa na maradhi au tabia ya kupenda kutembea uchi, kitaalamu inaitwa Exhibitonism. Wataalamu wa saikolojia wanasema maradhi hayo yanatawaliwa zaidi na akili, hayawezi kutibika kwa vidonge zaidi ya ushauri nasaha.
Wema
Linah
Ni maradhi au tabia ambayo mtu huona raha kuonekana sehemu zake za mwili zisizotakiwa kuonekana hadharani. Watu wa aina hiyo ni wale wanaopenda kuvaa vinguo vifupi kupita kiasi, na kutembea mitaani bila ya kuona aibu. Au kufanya maonyesho ya burudani katika shoo, katika sherehe mbali mbali za utoaji tuzo na katika video za muziki.
Aunty Ezekiel
Shilole
Mtu mwenye maradhi au tabia hiyo, kitaalamu anaitwa Exhibitionist. Tabia au maradhi ya kuwa na wendawazimu wa kupenda kuvaa nguo fupi sana, au kuvaa nusu uchi.
Ndauka
Lulu
Hivi sasa yameanza kuingia kwa kasi zaidi katika jamii yetu. Waigizaji na wanamuziki wa kitanzania wametokea kuvaa mavazi ya nusu uchi.
Ini Edo
Hamisa
Uwoya
Saturday, February 16, 2013
Movie Kitanzania bila mastaa haziuziki?
Baadhi ya wasambazaji wa sinema nchini, wameibuka na kituko kitakachosambaratisha soko la sinema za kibongo, kama hawatakubali kuachana na mawazo yao mgando ya kudai sinema bila ya msanii maarufu huwezi kuuza.
Uchunguzi wetu umeonyesha kabla ya kuwa na wasanii maarufu, watanzania walikuwa wakinunua sinema na kuangalia, wapo waliokuwa wakinunua sinema za kihindi bila ya kuwafahamu waigizaji hao kama maarufu au sio maarufu.
Wapo waliokuwa wakinunua sinema za kichina, kijapan na kizungu. Baada ya kuingia sinema za kinaigeria watanzania walizinunua, walipokuwa wananunua hawakujua kama wasanii hao ni maarufu, ila walinunua kwa ajili ya kupata burudani ya sinema.
Kama wasambazaji wa nchi nyingine wangekuwa na mawazao kama ya wasambazaji wetu. Tusingeshuhudia waigizaji wapya wakiibuka kila kukicha. Tungeendelea kushuhudia wale wale wa zamani ambao umri umeanza kuwatupa mkono.
Wasambazaji wanatakiwa kufahamu kama waigizaji wanaitwa mastaa hivi sasa, kuna watu wamewafikisha hapo, hawakuzaliwa wakiwa mastaa. Mnatakiwa na nyinyi kuzalisha wapya sio kutafuta mastaa walitengenezwa na wenzenu.
Bongo movie, Sound of Death inaoongoza kwa mastaa wengi Tanzania
Tumaini Bigirimana
Jacob Steven
Patcho Mwamba
Hemed Suleiman
Auntie Ezekiel
Yusufu Mlela
Sinema iliyotungwa na kuandikwa script na Haji Dilunga kisha kuongozwa na Mtitu G Game, inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya waigizaji maarufu hapa nchini.
Swahili Cinema News ilishuhudia mabishano makali ya wapenzi na mashabiki ya sinema za kibongo katika kibanda cha video.
Mabishano hayo yalidai Sound of Death ni sinema pekee iliyokusanya waigizaji wengi wenye majina makubwa hapa bongo.
Miongoni mwa majina ya waigizaji walioshiriki katika movie hiyo ya aina yake ni pamoja na Auntie Ezekiel, Jacob Steven, Rose Ndauka, Hemedi Suleiman, Flora Mvungi, Yusuf Mlela, Tumaini Bigirimana, Patcho Mwamba, Mayasa Mrisho.
Wengine ni Hidaya Njaidi, Tito, Masinde, Grace Mapunda, Mariam Georger, Abdul Ahmed a.k.a Ben, Bakari Makuka, Maua na wengine
Mpaka mwanahabari anaondoka hapo hakuna mshindi wa mabishano hayo, ila utafiti wetu umefanikiwa kugundua kwamba Sound of Death inaweza kuwa miongoni mwa sinema iliyokusanya idadi kubwa ya waigizaji wenye majina makubwa kwa mwaka 2012.
Subscribe to:
Posts (Atom)





















