Sunday, March 1, 2015

Viatu vya kishetani, ukivaa unamsambaza kwa nguvu moja.


          

               
Ukivaa unaendelea kumtukuza na kumsambaza shetani kwa wengi,    sio kila kinachotengenezwa na wabunifu ni  lazima ukivae.  Vitu vingine vinatengenezwa kwa sababu maalumu, watengenezaji wanajua wanachofanya, hakuna anayebahatisha katika hilo. Miongoni mwa wabunifu na watengenezaji wa mitindo mbali mbali ni wafuasi wa dini ya shetani. Kuweni makini katika kuchagua aina gani ya kiatu unachotaka kuvaa. Hasa kina dada wanaongoza kwa kuwa na mitindo mingi ya viatu na nguo.  Kwa vile wabunifu wanajua kama waigizaji, wanamuziki na wanamitindo wa mavazi ni watu wanaotazamwa sana na jamii, wanawavisha viatu hivyo kwa lengo la kuvitafutia soko na umaarufu miongoni mwa jamii ili shetani aweze kuwa na nguvu. Hivi sasa viatu hivyo vimeanza kutumika sana katika sinema mbali mbali au katika baadhi ya video za wanamuziki maarufu. Wakati mwingine vimekuwa vikitumika katika majukwaa ya wanamitindo. lengo ni kusambaza nguvu za shetani. kuwa makini kama unapenda kuigi kila kitu.

No comments:

Post a Comment