Showing posts with label Mwigizaji. Show all posts
Showing posts with label Mwigizaji. Show all posts

Tuesday, September 27, 2016

MWAJUMA AU MAIMUNA amefariki dunia


Huwezi kuamini lakini ndio hivyo imetokea, jumapili ya tarehe 28 mwezi wa nane, ni siku tuliyompoteza msanii mkongwe Mwajuma Abdul maarufu kwa jina la MAIMUNA. Akazikwa jumatatu tarehe 29 saa kumi katika makaburi ya kisarawe. kwa wale wanaofuatilia matangazo ya redio watamkumbuka kwa tangazo la HII SASA SIFAAA, NA LEO TENA NYAMAAA, ni miongoni mwa matangazo kati ya mengi aliyocheza. Katika televisheni anakumbukwa kwa matangazo mengi aliyofanya ila kwa haraka tangazo la kifua kikuu akiwa na Kaboba, Onyango na wengine. Baadhi watamkumbuka kwa michezo ya redio, hasa mchezo wa TWENDE NA WAKATI uliokuwa ukirushwa na redio Tanzania kwa sasa TBC. Kwa upande wa sinema ameshiriki sinema nyingi baadhi Ni UWANJA WA DHAMBI. Jina la MAIMUNA alilipata baada ya kushirikia katika sinema ya UWANJA WA DHAMBI, sinema iliyompatia umaarufu mkubwa. Baadhi ya sinema alizoshiriki ni pamoja na I LOVE YOU, LAZIMA UFE JORAM, PICNIC, BUNGE LA WACHAWI, POPOBAWA, ZINDIKO, BOSS nk. Pia aliwahi kushiriki tamthilia ya HUKUMU YA TUNU akitumia jina la TUNDA. Amefariki akiwa tayari amecheza sinema inayoendelea kueditiwa pamoja na Tamthilia inayoendelea kueditiwa. Amefariki ghafla hakuwa na maradhi yoyote, alikuwa mzima wa afya njema. Mpaka saa mbili usiku alikuwa mzima wa afya katika sherehe ya kitchen part ya ndugu yake, Ghafla alijisikia kuishiwa na nguvu na kuanza kutapika, hali hiyo iliendelea mpaka alivyokimbizwa Amani Hospital, hatimaye akafariki dunia muda mfupi.Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un

Sunday, February 1, 2015

Mwigizaji wa Nigeria Muna Obiekwe amefariki


                                                                       
             Marehemu  Muna Obiekwe wakati wa uhai wake, wengi watamkumbuka kwa uigizaji wake
 Marehemu Muna Obiekwe akifikishwa hospital kwa ajili ya matibabu baada ya kuzidiwa na ugonjwa, hata hakuweza kupona, umauti ukamfika
Picha hii ya Marehemu Muna Obiekwe ilionekana katika kituo cha Televvisheni, kilichokuwa ionaelezea kifo chake.

HABARI kutoka Nigeria zimesema mwigizaji maarufu wa kiume wa sinema nchini humo, Muna Obiekwe, amefariki jana katika hospitali ya Festac, jijini Lagos, baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa figo. Vyanzo vilivyokuwa karibu na mwigizaji huyo, vinasema Muna alikuwa akipambana na matatizo ya figo ambayo alikuwa ameyafanya siri kwa muda mrefu kabla ya kumwambia rais wa chama cha waigizaji cha Nigeria (AGN), Ibinabo Fiberesima,  ambaye aliendelea kuwa karibu naye.Habari hizo zinasema kwamba tabia ya kutumia sana vileo ya mwigizaji huyo ambaye makazi yake yalikuwa katika mji wa Enugu,  inaweza isihusiane na matatizo yaliyosababisha kifo chake. Muna atakumbukwa katika baadhi ya filamu zake kama: He Lives in Me, Songs Of Sorrow, Enemies in Love, It’s Juliet or No One, Wasted Effort na zinginezo.Msanii mwenzake kutoka Nollywood, Nonso Diobi, amethibitisha kifo hicho baada ya kuwepo sintofahamu kutoka kwa baadhi ya watu waliokuwa wakiweka taarifa katika mtandao wa Twitter kuwa Muna hajafariki. Nonso amethibitisha kifo hicho baada ya kuwasiliana na rais wa chama cha waigizaji cha Nigeria (AGN), Ibinabo Fiberesima na kuwataka watu waliokuwa wakipotosha kuhusu kifo hicho kuacha mara moja.

Friday, January 30, 2015

Mwigizaji raia wa Uingereza Dave Legeno amefariki

Mwigizaji raia wa Uingereza aliyecheza series za Harry Potter ‘Dave Legeno’ amekutwa amekufa jijini California, kwa mujibu wa The Hollywood Reporter. Dave Legeno, mwenye umri wa miaka 50, alikutwa akiwa amepoteza maisha siku ya Jumapili na mwili wake kuchukuliwa na helicopter.

Monday, December 1, 2014

Mwigizaji Bollywood azabwa kofi kwa kuvaa nguo fupi


                                                                   
                                                                   Gauhar Khan
                                                                        Gauhar Khan
                                                                    Gauhar Khan
                                                                    Gauhar Khan
                                                                          Gauhar Khan
                                                                 Gauhar Khan

Mwigizaji maarufu wa Bollywood ambaye pia ni mwanamitindo, Gauhar Khan, alizabwa kofi wakati wa shughuli ya kurekodi makala ya kipindi kuhusu maisha yake.
Mwigizaji huyo alizabwa kofi na mmoja wa waliokuwa wanatazama kipindi hicho eti kwa kuwa alikuwa amevalia nguo fupi sana.
Polisi walimkamata mwanamume mwenye umri a miaka 24 kwa kumshambulia mwigizaji huyo wakati wa kurekodi kipindi kijulikanacho kama , ''India's Raw Star'' mjini Mumbai.
Mwanamume aliyemshambua muigizaji huyo alinukuliwa akimkaripia na kumwambia, kwamba kwa kuwa yeye ni mwanamke wa kiisilamu hapaswi kuvalia nguo fupi kama ile.
Mwanamume huyo alitarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu.
Tukio hilo lilitokea Jumapili, wakati wa kurekodiwa kwa makala ya mwisho ya kipindi hicho.
Uchunguzi umeonyesha kuwa mtu mmoja kutoka kwa mashabiki, alianza kumkejeli Khan ambaye naye hakumsaza kwani alianza kujibizana naye. Katika majibizano yao, mwanamume huyo alimzaba kofi Khan.
Duru zinasema kuwa walinzi waliokuwa katika eneo hiloi walimshinda nguvu mwanamume huyo ambayo walimkabidhi kwa polisi.
Polisi walimshitaki mwanamume huyo kwa kitendo cha kumzaba kofi Khan ambaye ameigiza katika filamu nyingi tu ikiwemo, 'Rocket Singh: Salesman of the Year.'

Friday, November 28, 2014

Jacky Wolper mkali wa mapozi kuliko wenzake nchini Tanzani

                                                                
                                                   Wolper  pozi hili kama sio yeye
                                                              Wolper, hapa utakubali yeye
                                                       Wolper, na hapa mnasemaje alivyopozi
                                                           Hapa unasemaje jamani
                                                         Ametulia kama hataki kuongea
                                                 Anaonekana ana mawazo vile.

Tukubali au tubishe ukweli utabaki vile ulivyo kama mwanadada Jacky Wolper  ni mwigizaji wenyewe mapozi ya kipekee,  mapozi yake yanamuongeze mvuto wa hali ya juu katika picha zake anazopiga mara kwa mara. Baadhi ya watu wamesikika wakisema kwamba Wolper ni mkali wa mapozi katika upigaji wa picha tofauti  kuliko waigizaji wenzake. Na ndiyo maana aliweza kuchukua ushindi wa mwanamke mwenye mvuto. Hebu tazama picha hizi utagundua kama huyu binti ni mkali wa mapozi.

Saturday, July 13, 2013

Nikifa sitaki nikumbukwe kama mwigizaji- Eucharia




                                                             Eucharia Anunobi Ekwu
Lagos, Nigeria
Mwanamama nyota wa sinema za Nollywood Eucharia Anunobi Ekwu  ameachana na uchezaji wa sinema na kuamua kuokoka, kumtumikia mungu kwa muda wa maisha yake yaliyobaki hapa duniani.
Hivi karibuni  Euchari alitangaza kuachana na uigizaji na kuamua kumrudia mungu kwa kuokoka baada ya kutamba kwa sana katika sinema nyingi alizoshiriki kuigiza.
Katika mahojiano yake na kituo kimoja cha televisheni cha hapa Nigeria, Eucharia amesema  akifariki dunia akumbukwe kama aliwahi kuwa mwigizaji wa sinema.
"Ingawa nimecheza muvi nyingi kwa muda mrefu, lakini nasema wazi kwamba, nikifa nsikumbukwe kama msanii bali ni mtu wa mungu ambaye nimeamua kumtumikiakwa kipindi cha maisha yangu yote yaliyobaki duninai,"alisema mwanadada huyo mwenye mvuta wa kimapenzi na macho ya kuita.
Euchari atakumbukwa na wapenzi na mashabiki katika sinema ya Abuja Connection, sinema hiyo ameshirikiana kuigiza na wakali wengine kama Clarion Chukwura Abiola, Ngozi Ezeonu, Chidi Mokeme Enabeli Elabuwa na wengine wengi wenye majina makubwa Nigeria.
Sinema ilitungwa na Ojiofor Ezeanyaeche, script iliandikwa na Adim Williams sambamba na kuongozwa na Adim Williams mwenyewe.

Tuesday, February 19, 2013

Movie Tanzania, Inawezekana kila mwigizaji kutayarisha sinema?

  Inawezekana kila mwigizaji kuwa mtayarishaji wa sinema. Jibu linaweza kuwa ndio au hapana, kwa sababu utayarishaji wa sinema unaweza kufanywa na mdau yoyote mwenye uwezo wa fedha, ila awe anajua sanaa ya sinema kwa undani zaidi. Vinginevyo anaweza kuingia mikononi mwa wababaishaji na kujikuta akipoteza muda na fedha.

Mwigizaji anaweza kutayarisha sinema ila ni lazima awe na upeo mkubwa wa kutayarisha sio kuigiza, unaweza kuwa mwigizaji mzuri lakini ukashindwa kuwa mtayarishaji au muongozaji mzuri yaani director mzuri.

Wapo madirector wazuri sana, lakini hawawezi kuigiza. Kwa sababu hawana taranta au tunaweza kuita kipaji, wapo waandishi wazuri wa hadithi na vitabu, lakini hawawezi kuandika script.

Wapo wachezaji wazuri wa soka lakini hawezi kuwa makocha wazuri, wapo makocha wazuri lakini hawakuwahi kucheza mpira kwa kiwango cha kuitwa mastaa. Kwa hiyo ni vizuri kujikagua kama una taranta kabla ya kufanya chochote unachotaka kufanya.

Wapo waigizaji wenye taranta ya kutayarisha sinema na kuziongoza vizuri, mfano mwigizaji Mel Colm Cille Gerard Gibson wa Marekani, wengi wanamfahamu kwa Mel Gibson ni mwigizaji, mtayarishaji, mwandishi wa script na muongozaji. Moja ya sinema aliyoongoza ni Apocalypto

Marekani na Ulaya wapo wengi wenye uwezo wa kufanya yote katika utengenezaji wa sinema, pia wapo ambao hawawezi. Wanatoa nafasi kwa wenzao wanaoweza.
Kwa Tanzania hali ni tofauti, wengi hawawezi kutayarisha sinema wala kuziongoza. Ila wanajilazimisha kufanya hivyo kwa sababu wanajiona mastaa, ukweli unabaki kama sinema wanazotayarisha zinakuwa hazina ubora unaotakiwa.

Ukijiona huna uwezo wa kuandika script, kutayarisha na kuongoza. Tafuta wadau wenye uwezo wa kufanya kazi hizo kwa ajili ya kupata sinema nzuri. Matokeo ya kila kitu kutaka kufanya mwenyewe ni kutayarisha kazi mbovu.

Aliyekupa fedha za kutayarisha sinema akigundua sinema yako haipendwi na watazamaji, atakumwaga na hatimaye kupotea katika soko la sinema kabisa.

Kama lengo la wadau ni kuendeleza sekta ya uigizaji, waigizaji wanaopata bahati ya kuingia mikataba na wasambazaji kwa ajili ya kutayarisha sinema, wasiwe wabinafsi. Kuendekeza ubinafsi ni kuua sekta sinema, inayoongoza hivi sasa kwa kutoa ajira kwa vijana na wazee.
 
 
 
 

Saturday, February 16, 2013

Camera man, mwigizaji wanapokuwa madirector



                                                                   Camera man
Imekuwa kawaida katika nchi yetu ya Tanzania kumsikia  camera man au mwigizaji akibishana na Director.  Ugonjwa huu usipokemewa unaweza kuambukiza kizazi kijacho katika sanaa ya sinema.

Kitaalamu  production yote ipo chini ya director,  yeye  ndiye mwenye maamuzi ya mwisho. Anapoamua  jambo lolote hakuna mwenye ubavu wa kubisha, mliokuwa hapo mnaweza kumpa ushauri,  ni maamuzi yake kukubali au kukataa.

Mfano mzuri  director ni kocha wa timu ya mpira,  huwezi kuingilia maamuzi ya kochi katika kutayarisha kikosi chake.

Kwa upande wa utayarishaji wa sinema  madirector wanaingilia katika kufanya maamuzi yao,  matokeo yake wanajikuta wanatayarisha sinema  yenye makosa. 

Makosa yenye yanasababishwa na kutokuwa makini. Mwigizaji anambishia director, camera man anambishia director anajifanya anajua sana,  matokeo ya mabishana hayo ni Director kupoteza umakini na kufanya kazi mbovu.

Camera man  na waigizaji  tuwaache  madirector wafanye kazi zao,  kuwaingilia kuna sababisha kuendelea kushuhudia sinema zenye mapungufu na makosa ya kijinga, ambayo hayahitaji  elimu ya chuo kikuu kuweza kuyabaini.

Kama wewe mwigizaji fanye kile ulichokufikisha pale, mambo ya kuelekeza hayakuhusu. Nawe camera man fanye kazi yako ya kupiga picha, kuelekeza waigizaji namna ya kucheza sio kazi yako. Hiyo ni kazi ya Director na msaidizi wake.

Kila mmoja akizingatia jukumu lake, makosa ya kipumbavu katika sinema zetu yatapungua.  Ushauri kwenu wenye tabia hizo, kusema  ACTION   na CUT sio sababu ya kujiona unaweza kudirect movie.

Kuidirect movie ni zaidi ya ACTION  na CUT,  tuwape nafasi  madirector kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi. Unajua kama kusimama nyuma ya camera sio sababu ya kuitwa camera man, au kubeba  jezi na mpira sio kigezo cha kuitwa mchezaji. Au kubeba gitaa sio sababu ya kuitwa mwanamuziki. Au kushinda kutwa chumba cha habari huwezi kuitwa mwandishi au mtangazaji. Unaweza kuwa mfagiaji.