Camera man
Imekuwa kawaida katika nchi yetu ya Tanzania kumsikia camera man au mwigizaji akibishana na
Director. Ugonjwa huu usipokemewa
unaweza kuambukiza kizazi kijacho katika sanaa ya sinema.
Kitaalamu production
yote ipo chini ya director, yeye ndiye mwenye maamuzi ya mwisho.
Anapoamua jambo lolote hakuna mwenye
ubavu wa kubisha, mliokuwa hapo mnaweza kumpa ushauri, ni maamuzi yake kukubali au kukataa.
Mfano mzuri director
ni kocha wa timu ya mpira, huwezi
kuingilia maamuzi ya kochi
katika kutayarisha kikosi chake.
Kwa upande wa utayarishaji wa sinema madirector wanaingilia katika kufanya maamuzi
yao, matokeo yake wanajikuta wanatayarisha
sinema yenye makosa.
Makosa yenye yanasababishwa na kutokuwa makini. Mwigizaji
anambishia director, camera man anambishia director anajifanya anajua sana, matokeo ya mabishana hayo ni Director
kupoteza umakini na kufanya kazi mbovu.
Camera man na
waigizaji tuwaache madirector wafanye kazi zao, kuwaingilia kuna sababisha kuendelea
kushuhudia sinema zenye mapungufu na makosa ya kijinga, ambayo hayahitaji elimu ya chuo kikuu kuweza kuyabaini.
Kama wewe mwigizaji fanye
kile ulichokufikisha pale, mambo ya kuelekeza hayakuhusu. Nawe camera man fanye
kazi yako ya kupiga picha, kuelekeza waigizaji namna ya kucheza sio kazi yako.
Hiyo ni kazi ya Director na msaidizi wake.
Kila mmoja akizingatia jukumu lake, makosa ya kipumbavu
katika sinema zetu yatapungua. Ushauri
kwenu wenye tabia hizo, kusema
ACTION na CUT sio sababu ya
kujiona unaweza kudirect movie.
Kuidirect movie ni zaidi ya ACTION na CUT,
tuwape nafasi madirector kufanya
kazi zao kwa uhuru zaidi. Unajua kama kusimama nyuma ya camera sio sababu ya
kuitwa camera man, au kubeba jezi na
mpira sio kigezo cha kuitwa mchezaji. Au kubeba gitaa sio sababu ya kuitwa
mwanamuziki. Au kushinda kutwa chumba cha habari huwezi kuitwa mwandishi au
mtangazaji. Unaweza kuwa mfagiaji.
No comments:
Post a Comment