Wadau wa sinema wanashindwa kuelewa kama waandishi wa script
ni kiungo muhimu sana katika utayarishaji wa sinema. Bila ya
script huwezi kupata sinema, bila ya script huwezi kujua uwezo wa mwigizaji au
director.
Mwandishi wa script anakuwa tayari ametayarisha sinema
kimaandishi, waigizaji na director wanaitoa kwenye maandishi na kuiweka kivitendo.
Kila kinachofanywa na waaigizaji katika sinema husika kimetoka katika akili ya mwandishi wa script.
Cha ajabu waandishi na watangazaji wanawasahau
waandishi wa script na kutoa nafasi kubwa kwa waigizaji. Kitendo hicho
kinachangia kuifanya jamii kutofahamu umuhimu wa waandishi wa script.
Angalau madirector wanapata nafasi ya kutangazwa katika
vyombo vya habari, waandishi script bado hawajapata nafasi hiyo, lakini hata madirector wanapata nafasi finyu sana ukilinganisha na
waigizaji.
Madirector wanaopata nafasi katika vyombo vya habari ni wale
wanaodirect na kuigiza, kwa wale wanaodirect
bila ya kuigiza bado wananafasi finyu katika vyombo vya habari.
Ikiwa kwenye muziki,
mtayarishaji (Producer ) anapata nafasi
kubwa katika vyombo vya habari, inashindikana
vipi kwa madirector, maproducer,
mascript writer wa sinema kupata nafasi
kubwa kama wanavyopata waigizaji au watayarishaji wa muziki.
Imefika wakati wa
vyombo vya habari kubadili na kuandika
taarifa za madirector, maproducer na waandishi wa script.
Tatizo kama hili lipo kwenye muziki wa taarabu, anayetunga wimbo, muziki na wapigaji vyombo
hawapewi nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari kuliko waimbaji.
Badilikeni wadau wa vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment