Showing posts with label Director. Show all posts
Showing posts with label Director. Show all posts

Saturday, February 16, 2013

Vyombo vya habari vyawasahau Producer, Director na Script writer



Wadau wa sinema wanashindwa kuelewa kama waandishi wa script ni  kiungo muhimu sana katika utayarishaji wa sinema. Bila ya script huwezi kupata sinema, bila ya script huwezi kujua uwezo wa mwigizaji au director.

Mwandishi wa script anakuwa tayari ametayarisha sinema kimaandishi, waigizaji na director wanaitoa kwenye maandishi na kuiweka kivitendo.

Kila kinachofanywa na waaigizaji katika sinema husika  kimetoka katika akili ya mwandishi wa script. Cha ajabu  waandishi na watangazaji  wanawasahau  waandishi wa script na kutoa nafasi kubwa kwa waigizaji. Kitendo hicho kinachangia kuifanya jamii kutofahamu umuhimu wa waandishi wa script.

Angalau madirector wanapata nafasi ya kutangazwa katika vyombo vya habari, waandishi script bado hawajapata nafasi hiyo,  lakini hata madirector wanapata nafasi finyu sana ukilinganisha na waigizaji.

Madirector wanaopata nafasi katika vyombo vya habari ni wale wanaodirect na kuigiza, kwa wale wanaodirect  bila ya kuigiza bado wananafasi finyu katika vyombo vya habari.

Ikiwa kwenye  muziki, mtayarishaji (Producer )  anapata nafasi kubwa katika vyombo vya habari, inashindikana  vipi kwa  madirector, maproducer, mascript writer  wa sinema kupata nafasi kubwa kama wanavyopata waigizaji au watayarishaji wa muziki.

Imefika  wakati wa vyombo vya habari kubadili na kuandika  taarifa za madirector, maproducer na waandishi wa script.

Tatizo kama hili lipo kwenye muziki wa taarabu,  anayetunga wimbo, muziki na wapigaji vyombo hawapewi  nafasi kubwa  kwenye vyombo vya habari kuliko  waimbaji.  Badilikeni wadau wa vyombo vya habari.

Madirector wanachangia muvi kukosa uhalisia



Mwigizaji wa sinema ya Julio na Romeo, Nurati Ngeleshi alisikika akiwashutumu waongozaji wa movie a.k.a madirector kwa kushindwa kuwalazimisha waigizaji kuvaa uhusika wa nafasi wanazocheza.

Hakuna kitu kinachonikera kama waigizaji wa kike kuvaa vimini sehemu hisiyostahili."  Akasema director mwenye umakini na kazi hawezi kukubali kitu kama hicho.

Inawezekana alichoongea Nurati kitawaboa wengi, ukweli utabaki pale pale kama madirector wanachangia kupoteza uhalisia wa sinema zetu kwa kuogopa kuwaeleza waigizaji ukweli wa kuvaa taswira ya nafasi aliyopewa.

Katika utayarishaji wa sinema director ni mtu wa mwisho katika kufanya maamuzi. Hakuna mtu yoyote anayeweza kupinga maamuzi ya director, yeye ndiye mwenye mtazamo wa taswira wa sinema anayotaka kuitengeneza, na aina ya waigizaji na mavazi wanayotakiwa kuvaa.

Mwisho wa yote sinema ikitoka mbovu anaulizwa yeye sio muigizaji, kwa hiyo waongozaji kama sio madirector wanatakiwa kuwa makini sana.