Mwigizaji
wa sinema ya Julio na Romeo, Nurati Ngeleshi alisikika akiwashutumu waongozaji
wa movie a.k.a madirector kwa kushindwa kuwalazimisha waigizaji kuvaa uhusika
wa nafasi wanazocheza.
“Hakuna kitu kinachonikera
kama waigizaji wa kike kuvaa vimini sehemu hisiyostahili." Akasema director mwenye umakini na kazi
hawezi kukubali kitu kama hicho.
Inawezekana
alichoongea Nurati kitawaboa wengi, ukweli utabaki pale pale kama madirector wanachangia
kupoteza uhalisia wa sinema zetu kwa kuogopa kuwaeleza waigizaji ukweli wa
kuvaa taswira ya nafasi aliyopewa.
Katika
utayarishaji wa sinema director ni mtu wa mwisho katika kufanya maamuzi. Hakuna
mtu yoyote anayeweza kupinga maamuzi ya director, yeye ndiye mwenye mtazamo wa
taswira wa sinema anayotaka kuitengeneza, na aina ya waigizaji na mavazi
wanayotakiwa kuvaa.
Mwisho wa yote sinema
ikitoka mbovu anaulizwa yeye sio muigizaji, kwa hiyo waongozaji kama sio
madirector wanatakiwa kuwa makini sana.
No comments:
Post a Comment