Monday, February 11, 2013

Stella ni zao la Alwatan Artist Theater Tanzania



Stella Baltazar


Msanii anayenyemelea kuwa mkongwe katika fani ya sinema, Stella Baltazar ni zao la kikundi cha Alwatan Artist Theater.

Stella aliletwa kampuni ya Heko Production na Marehemu Salum Karanda kwa la kucheza sinema inayoitwa Mikono mwa nunda, wakati huo alikuwa hajawahi kushiriki kikundi chochote cha sanaa.

Kwa vile Stella alikuwa na vitu vitano ambayo A, B, C, D, E. kwa ufanunuzi ni kwamba A for appearance, B for body structure, C for civilization, D for discipline na E for education, alipatia nafasi ya kucheza kama Nunda, msichana anayeua watu na kujidai ni Nunda mla watu.

Kwa bahati mbaya sinema hiyo haikuweza kutayarishwa. Mzee Karanda alimchukua tena na kumfikisha kikundi cha Alwatan, Uongozi wa kikundi ulimpokea na kumfundisha mbinu mbali mbali za kuigiza

Sinema yake ya kwanza ilikuwa Uwanja wa Dhambi aliyocheza kwa jina la Shubiri. Sinema ya pili ilikuwa I love you aliyocheza kwa jina la Sophia.

Baada ya hapo aliamua kujiunga na kikundi cha Shirikisho kilichokuwa kinarusha tamthilia yake televisheni ya ITV.
Katika tamthilia hiyo alikuwa akitumia jina la Kitalansi, baadaye alijikuta akipata nafasi ya kushiriki sinema zilizotayarishwa na kampuni ya Game first Quality Tanzania. Huko alicheza sinema nyingi kama vile Red Valentine na nyingine nyingi.






No comments:

Post a Comment