Jamila chipukizi anayekuja juu
Baadhi ya wasambazaji wa sinema nchini,
wameibuka na kituko
kitakachosambaratisha soko la sinema za kibongo, kama hawatakubali kuachana na mawazo yao mgando ya kudai sinema bila ya
msanii maarufu huwezi kuuza.
Uchunguzi wetu
umeonyesha kabla ya kuwa na wasanii
maarufu, watanzania walikuwa wakinunua
sinema na kuangalia, wapo waliokuwa
wakinunua sinema za kihindi bila ya kuwafahamu waigizaji hao kama
maarufu au sio maarufu.
Wapo waliokuwa wakinunua sinema za kichina, kijapan na
kizungu. Baada ya kuingia sinema za kinaigeria watanzania walizinunua, walipokuwa wananunua hawakujua kama wasanii hao ni maarufu, ila walinunua kwa ajili ya
kupata burudani ya sinema.
Kama wasambazaji wa nchi nyingine wangekuwa na mawazao kama ya wasambazaji wetu. Tusingeshuhudia waigizaji wapya wakiibuka kila kukicha.
Tungeendelea kushuhudia wale wale wa zamani ambao umri umeanza kuwatupa
mkono.
Wasambazaji wanatakiwa kufahamu kama
waigizaji wanaitwa mastaa hivi sasa, kuna watu wamewafikisha hapo, hawakuzaliwa wakiwa mastaa. Mnatakiwa na
nyinyi kuzalisha wapya sio kutafuta mastaa walitengenezwa na wenzenu.
No comments:
Post a Comment