Showing posts with label bongo. Show all posts
Showing posts with label bongo. Show all posts

Friday, November 28, 2014

Wema bado ni kipenzi cha wabongo kila anachofanya wanashabikia

                                                                        
                                                      
Bila ya kupindisha ukweli mwigizaji Wema Sepetu ni miongoni mwa waigizaji wenye nyota kali sana kwa wapenzi na mashabiki,  ukitaka kudhibitisha hilo angalia magazeti ya udaku yakiwa na picha yake sambamba na stori yake. watu wengi kwenye daladala utawaona wanamagazeti hayo wanasoma. Udhibitisho mwingine angalia idadi ya wasomaji na watazamaji wa video zinazomuhusu yeye  katika blog mbali mbali ni kubwa kuliko waigizaji wengine.  Udhibitisho mwingine jaribu kuchungu wale watu waliokuwa karibu yake walivyojipatia umaarufu kubwa, baada ya kuachana nao wengi wao wanapoteza umaarufu.  Kama unataka kuwa maarufu jipendekeze kwa  Wema hata kwa kubeba mkoba wake au kumfuta jasho, siku tatu ya kuwa naye tayari utapamba katika kurasa za magazeti ya udaku. Wema bado ni kipenzi cha wabongo, habari ndiyo.

Saturday, July 13, 2013

Auntie Ezekiel aibuka kwenye bongo fleva

                                                   Auntie Ezekiel katika moja ya pozi lake
                                                    Auntie Ezekiel katika  pozi jingine

Baada ya kujipatia umaarufu mkubwa katika uigizaji, mwanadada nguli katika uigizaji wa sinema za kibongo, Auntie Ezekiel ameamua kujikita katika muziki, baada ya kushirikishwa kwenye wimbo unaoitwa Movie Star wa January Joseph a.k.a January Eleven.
Kwa mujibu wa maelezo yake, Auntie Ezekiel amesema ana mambo mengi anayotaka kufanya katika muziki, ila kwa sasa hajawa tayari kuweka wazi mambo hayo. Ila anasubiri kuona namna mashabiki watakavyompokea.
"Nimeamua kuwaonyesha mashabiki na wapenzi wangu kwamba ninaweza kufanya muziki, kama nikubalika nitaamua kujiingiza moja kwa moja kwenye muziki. Ila naamini kama nitapokewa vizuri na kukubakli," alisema nyota huyo wa sinema ya Sound of death.
Kama Auntie Ezekiel ataingia moja kwa moja katika muziki, atakuwa anaungana na waigizaji wengine walioamua kujiingiza kwenye muziki kama vile Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole, Salma Jabu maarufu kama Nisha, Flora Mvungi na Snura Mushi. 

Saturday, February 16, 2013

Bongo movie, Sinema bila Staa huwezi kuuza




                                                         Jamila chipukizi anayekuja juu
Baadhi ya wasambazaji wa sinema  nchini,  wameibuka na  kituko kitakachosambaratisha soko la sinema za kibongo, kama  hawatakubali kuachana  na mawazo yao mgando ya kudai sinema bila ya msanii maarufu huwezi kuuza.

Uchunguzi  wetu umeonyesha  kabla ya kuwa na wasanii maarufu, watanzania walikuwa  wakinunua sinema na kuangalia,  wapo waliokuwa wakinunua sinema za kihindi bila ya kuwafahamu waigizaji hao kama maarufu au sio maarufu.

Wapo waliokuwa wakinunua sinema za kichina, kijapan na kizungu. Baada ya kuingia sinema za kinaigeria watanzania walizinunua,  walipokuwa wananunua hawakujua kama wasanii hao ni maarufu, ila walinunua kwa ajili ya kupata burudani ya sinema.

Kama wasambazaji wa nchi nyingine wangekuwa na mawazao kama ya wasambazaji wetu. Tusingeshuhudia  waigizaji wapya wakiibuka kila kukicha. Tungeendelea kushuhudia wale wale wa zamani ambao umri umeanza kuwatupa mkono. 

Wasambazaji wanatakiwa kufahamu kama waigizaji wanaitwa mastaa hivi sasa, kuna watu wamewafikisha hapo,  hawakuzaliwa wakiwa mastaa. Mnatakiwa na nyinyi kuzalisha wapya sio kutafuta mastaa walitengenezwa na wenzenu.


Friday, February 15, 2013

Anna Michael utakumbukwa daima kwenye Movie bongo, Tanzania




                                            Marehemu Anna Michael enzi ya uhai wake                                 
Jina kama Sina alilotambanalo katika kikundi cha Kidedea au Tunu alilovuma nalo katika sinema ya I love you,ni kilelezo tosha  kama uwezo wa Anna Michael katika sanaa ya kuigiza ulikuwa wa kiwango cha juu.

Majina hayo yalitaka kufuta jina lake halisi la Anna Michael, alilopewa na wazazi wake. Wahenga walisema kila kilichokuwa kizuri hakidumu sana, ni kauli inayowakilisha ukweli wa machungu yanayouma. Lakini yote ni mipango ya mwenyezi mungu.

Licha ya wazazi wake, mtoto wake, ndugu, marafiki, waigizaji wenzake, wapenzi na mashabiki wake walimpenda, lakini mungu alimpenda zaidi na kumchukua.

Ni miaka minne sasa tangu Anna Michael hatutoke kimwili na kiroho lakini kazi zake zitaendelea kuwepo katika maisha yetu ya kila siku.

Kila utakapotazama sinema ya Uwanja wa dhambi, I love you, Picnic na Confess. Utaweza kujionea kipaji alichobahatika kuwa nacho marehemu.

Wasanii wanaochipukia wangetafuta sinema alizocheza waweze kujifunza mambo muhimu.

Marehemu alikuwa anavaa taswira anayotakiwa kucheza, ni vigumu kwa sasa kupata wasanii wenye uwezo huo. Wengi wanapoteza uhalisi wanapoigiza.

Kuna wale wanaopoteza uhalisi wa sauti, muonekana na hata mavazi. Kazi kwenu wasanii chipukizi.