Showing posts with label Wema. Show all posts
Showing posts with label Wema. Show all posts
Friday, November 28, 2014
Wema bado ni kipenzi cha wabongo kila anachofanya wanashabikia
Bila ya kupindisha ukweli mwigizaji Wema Sepetu ni miongoni mwa waigizaji wenye nyota kali sana kwa wapenzi na mashabiki, ukitaka kudhibitisha hilo angalia magazeti ya udaku yakiwa na picha yake sambamba na stori yake. watu wengi kwenye daladala utawaona wanamagazeti hayo wanasoma. Udhibitisho mwingine angalia idadi ya wasomaji na watazamaji wa video zinazomuhusu yeye katika blog mbali mbali ni kubwa kuliko waigizaji wengine. Udhibitisho mwingine jaribu kuchungu wale watu waliokuwa karibu yake walivyojipatia umaarufu kubwa, baada ya kuachana nao wengi wao wanapoteza umaarufu. Kama unataka kuwa maarufu jipendekeze kwa Wema hata kwa kubeba mkoba wake au kumfuta jasho, siku tatu ya kuwa naye tayari utapamba katika kurasa za magazeti ya udaku. Wema bado ni kipenzi cha wabongo, habari ndiyo.
Friday, March 29, 2013
Wema na Jaquliane mfano wa kuigwa
Aliyewahi kuwa Miss Tanzania na mwigizaji maarufu nchini, Wema Sepetu amefanya tukio la kistarabu baada ya kumsaidia mwigizaji mwenzake Kajala Masanja kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka mitano baada ya kumlipia milioni kumi na tatu.
Kwa mujibu wa hukumu ya hakimu Sundi Fimbo wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Alimuhukumu Kajala kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya milioni kumi na tatu za kitanzania.
Wema alijitokeza kulipa faini hiyo, Kajala akajikuta akiwa uraiani akiwa huru. Mumewe alikosa mtu wa kumlipia faini alikuja akienda jela kutumikia kifungo.
Kitendo alichofanya Wema Sepetu kinafanana na kile alichofanya mwigizaji mwingine maarufu anayeitwa Jaquline Wolper kwa kutoa kiasi kikubwa fedha kusaidia matibabu ya marehemu Sajuki.
Waigizaji hawa ni mfano mzuri wa kuigwa, licha ya mapungufu yao. Kila binadamu ana mapungufu yake, cha muhimu kujiuliza yale mapungufu yao yanawaumiza wengine. Kama jibu hapana hatuna haki ya kuwasakama.
Tunatakiwa kuwapa moyo ili waweze kuendelea kusaidia wenzao, kutoa msaada sio suala la kuwa na fedha nyingi. Wapo watu wana fedha nyingi sana lakini hawatowi msaada kwa mtu yoyote.
Tukubali tusikubali Wema na Jaquliane ni mfano wa kuigwa. mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Wema na Jaquliane wanastahili pongezi.
Kama kweli walichofanya Wema na Jaquliane ni kitu cha kawaida, hawastahili kupongezwa. Mbona hatujaona kampuni yoyote ya usambazaji wa sinema kutoa kiasi kikubwa cha fedha kama hicho kuwasaidia wahusika. Wakati wao wana fedha nyingi kuliko Wema na Jaquliane, swali kwenu.
Tuesday, March 26, 2013
Wema amnusuru Kajara kwenda Jela
HUKUMU ya kesi iliyokuwa inamkabili staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mumewe imetolewa na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar. Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 213.
Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na msala wa kutaka kujipatia fedha haramu. Hata hivyo msanii Wema Sepetu amemwokoa Kajala kwa kumlipia faini ya shilingi milioni 13 ili kumnusuru na kifungo cha kwenda jela
Wema anawaongoza waigizaji wa kike
Baadhi ya wadau wa sinema wamesikika wakisema Wema Sepetu ni miongoni mwa waigizaji wanaopenda kuvaa viatu virefu kwa muda mrefu kuliko waigizaji wote wa kike.
Mabishano hayo yalitokea kwenye baa moja maarufu wakati wakiangalia sinema ya DJ BEN iliyochezwa na Jacob Stephen, Irene Uwoya na Wema Sepetu.
Jamaa mmoja iliyoonekana kulewa ilisikika ikiongea kwa sauti, Wema anaongoza kwa kuvaa viatu virefu. Kila utakapomuona iwe kwenye televisheni, magazeti au mtaani utamuona amevaa kiatu kirefu tofauti na waigizaji wenzake wa kike.
“ Ni kweli Wema anapenda kuvaa viatu virefu, ila atakuja kulia uzeeni. Miguu itamsumbua sana." alidai mwanamke mmoja aliyekuwa akipata ulabu katika baa hiyo.
“ Wema anaongoza wenzake, wapili nani na mwisho ni nani?" Aliuliza Mzee mmoja wa makamu huku akicheka kilevi.
“ Wa pili Lulu," Mlevi mwingine alijibu.“ Sio Lulu, yule mke wa Ndikumana." mwingine alijibu. “ Anaitwa Irene Uwoya." Alijibu huyo Mwanamke.
Shangazi Ezekiel akimanisha Auntie Ezekiel na Mrs Dallas akimanisha Jaquline Wolper mbona mmewasahau?" Yule Mzee wa makamu aliuliza.
Jamaa aliyeanzisha mada hiyo alidai wiki ijayo wakikutana hapo atawatajia wa pili na mwisho.
Swahilicinemanews tunakubalina na wadau kama mwanamke akivaa kiatu kirefu anapendeza. Kazi kwenu waigizaji wa kike kutinga viatu virefu kwa ajili ya kuvutia machoni mwa mashabiki wenu.
Subscribe to:
Posts (Atom)
