Showing posts with label Sinema. Show all posts
Showing posts with label Sinema. Show all posts

Tuesday, September 27, 2016

MWAJUMA AU MAIMUNA amefariki dunia


Huwezi kuamini lakini ndio hivyo imetokea, jumapili ya tarehe 28 mwezi wa nane, ni siku tuliyompoteza msanii mkongwe Mwajuma Abdul maarufu kwa jina la MAIMUNA. Akazikwa jumatatu tarehe 29 saa kumi katika makaburi ya kisarawe. kwa wale wanaofuatilia matangazo ya redio watamkumbuka kwa tangazo la HII SASA SIFAAA, NA LEO TENA NYAMAAA, ni miongoni mwa matangazo kati ya mengi aliyocheza. Katika televisheni anakumbukwa kwa matangazo mengi aliyofanya ila kwa haraka tangazo la kifua kikuu akiwa na Kaboba, Onyango na wengine. Baadhi watamkumbuka kwa michezo ya redio, hasa mchezo wa TWENDE NA WAKATI uliokuwa ukirushwa na redio Tanzania kwa sasa TBC. Kwa upande wa sinema ameshiriki sinema nyingi baadhi Ni UWANJA WA DHAMBI. Jina la MAIMUNA alilipata baada ya kushirikia katika sinema ya UWANJA WA DHAMBI, sinema iliyompatia umaarufu mkubwa. Baadhi ya sinema alizoshiriki ni pamoja na I LOVE YOU, LAZIMA UFE JORAM, PICNIC, BUNGE LA WACHAWI, POPOBAWA, ZINDIKO, BOSS nk. Pia aliwahi kushiriki tamthilia ya HUKUMU YA TUNU akitumia jina la TUNDA. Amefariki akiwa tayari amecheza sinema inayoendelea kueditiwa pamoja na Tamthilia inayoendelea kueditiwa. Amefariki ghafla hakuwa na maradhi yoyote, alikuwa mzima wa afya njema. Mpaka saa mbili usiku alikuwa mzima wa afya katika sherehe ya kitchen part ya ndugu yake, Ghafla alijisikia kuishiwa na nguvu na kuanza kutapika, hali hiyo iliendelea mpaka alivyokimbizwa Amani Hospital, hatimaye akafariki dunia muda mfupi.Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un

Wednesday, February 4, 2015

Sinema ya Bekitatu yatoa watu machozi


Unaweza kuona kama hadithi ya kufikirika, lakini tukio hili limetokea katika banda la video la maeneo ya Mwanagati, wilaya ya ilala, jimbo la Ukonga. Baadhi ya watu waliokuwa wakiangalia sinema hiyo walijikuta wakitokwa na machozi.
Kwa mujibu wa maelezo ya Kijana anayeonyesha video katika banda hilo, anayejulikana kwa jina Festo amesema alichukua DVD ya BEKITATU kwa kushawishiwa na muuzaji, hakutarajia kama itatokea kuwa nzuri kiasi cha kuvutia watu.
"Wengi wameingia katika banda langu kuangalia video ya Swagga ya JB, baada ya kumaliza kuonyesha sinema ya Swagga niliweka Bekitatu yenye waigizaji wanaochipukia, baada ya kuweka katika deki, baadhi  watu walinyanyuka na kutoka nje,  ila wengine waliendelea kuangalia." alisema.Baada ya kuanza sinema na kuonekana kijana akinyata  kwenda kubaka, vijana waliokuwa wanaangalia wakaanza kupiga makelele ya kushangilia, waliotoka nje wakaanza kurudi kuangalia. Kadri sinema ilivyozidi kuendelea watu walianza kuingiwa na huruma na kuanza kusifia kama waigizaji wamejitahidi.
"Binafsi sina kawaida ya kutokwa na machozi ninapoangalia sinema za kibongo. Ila Bekitatu ni sinema ya aina yake, unapoangalia huwezi kujua nini kitakachotokea mbele, kila hatua inakuvutia kutazama.
Kama kuna wanawake makatili, Rukia ni miongoni mwao, kwa upande wa Bekitatu amecheza vizuri sana, ameweza kupokea manyanyaso kwa kiwango cha juu kiasi cha kuwafanya watazamaji kumuonea huruma na hatimaye kutokwa na machozi. Vipande vilivyonipa machungu makubwa ni pale walipompiga kwa kumchangia, chakula chake kilipotiwa katika maji machafu, chungwa lake kukanyagwa na kulazimishwa kula. Nguo yake ilivyochomwa moto, alivyonyimwa mshahara wake, kukanyagwa na kiatu. Sehemu nyingine ni watoto wa Rukia walivyokuwa wanatapatapa kwa ajili ya sumu, Bekitatu alivyokamatwa, Rukia analilia watoto wake baada ya kugundua wamekufa. Nikitaja vipande vyote nitamailiza sinema, kipande kilichowachekesha watu ni kile cha kijiweni. Hasa yule kijana mchungaji alivyokuwa akichangia maongezi na wenzake." alisema Festo.

Tuesday, January 6, 2015

Picha za waigizaji waliocheza sinema ya Beki tatu



Hawa amecheza Bekitatu
Nurati amecheza Rukia
                                                                 Clemensia amecheza Leila

Rafael kama Polisi

Hassan kama Bakari
                                                                       Isaya  kama Iyama
Amecheza kama Bibi wa Bekitatu

Anna amecheza Nasra 
                                                           Mlekwa kama Mlinzi
 
Pascal kama Ramson
                                                                 Nurdin kama Jaffary
                                                                Joyce kama Joy
                                                           Kana kama Mlinzi











Nurati aibuka ndani ya Sinema ya Bekitatu

                                                         
                                                                 
Nurati Ngeleshi


Nurati Ngeleshi
Mwigizaji anayechipukia katika ulimwengu wa sinema nchini,  Nurati Ngeleshi a.k.a Belinda ameitaka serikali kuwasaidia kurahisisha upatikani wa vitendea kazi ili kuleta uhalisi katika sinema zao, sambamba na kutoa ushindani katika soko la kimataifa.
Kwa mujibu wa maelezo yake,  Belinda  amesema sinema nyingi zinazotayarishwa hivi sasa, hazina ubora na uhalisia kwa sababu ya kukosekana vitendea kazi na sehemu husika za kuigizia.
Amesema inakuwa vigumu kupata mavazi ya kweli ya polisi, jeshi, magereza na trafiki. Kukosekana kwa mavazi hayo kunachangia sinema zetu kupoteza uhalisi.
“Hebu angalia sinema za waafrika wenzetu kama Nigeria, Ghana, Kenya, Uganda na nchi nyingine. Utaona walivyopiga hatua katika kujenga uhalisia wa sinema zao kwa kutumia vitendea kazi husika na maeneo husika ya kuigizia" alisema Belinda.
Serikali ingesaidia watayarishaji kupata kwa urahisi mavazi ya askari wa aina zote, kutumia vituo vya polisi, majengo ya mahakama, bendera, majengo ya hospital za serikali sambamba na maofisi yake.
Kwa upande wa silaha, serikali ingeruhusu  bastola, bunduki na hata mabomu ya bandia kuingia nchini kwa ajili ya kurahisisha utayarishaji wa sinema kwa lengo la kuleta uhalisia.
Hivi sasa wengi wanatayarisha sinema kwa kutumia vibastola vya kuchezea watoto. Mtu yoyote akitazama anagundua kama ni kibastola cha watoto, ubora unapungua na uhalisia unapotea.
Belinda amewataka baadhi ya wadau na viongozi wa serikali, wasipende kulalamika kama sinema za kitanzania hazina uhalisia, eti kwa sababu wanavaa nguo fupi na kucheza sana kuhusu mapenzi. Kabla ya kulalamika walitakiwa kuitazama jamii ya kitanzania, wanaweza kupata majibu ya kwanini watayarishaji wanatengeneza sinema za kuvaa vimini na mapenzi.
Kwa kawaida mtayarishaji, mwandishi wa kitabu au mtunzi wa nyimbo, wana kawaida ya kutunga au kutengeneza yale mambo yanayotokea katika jamii yetu. Sio rahisi kutunga vitu vya kufikirika.
Kwa hiyo vimini na mapenzi ndivyo vinavyoendelea hivi sasa katika jamii yetu. Ndio maana sinema zinahusu mapenzi, nyimbo zinahusu mapenzi na vitabu vinahusu mapenzi.
Belinda ameitaka serikali kuweka utaratibu wa kuwakodisha waigizaji vitendea kazi vitakavyosaidia kuleta uhalisia na ubora tofauti na hivi sasa. Hata hivyo serikali inatakiwa kujua kama sinema imetoa na kuendelea kutoa ajira kwa watu wengi nchini.
Akizungumzia  maisha yake ya sanaa, anasema alizaliwa wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro. Sanaa alianza kuifanya  toka alivyokuwa shule,  baada ya kumaliza hakuendelea na mambo ya sanaa zaidi ya kujitumbukiza katika biashara.  Alikuwa akitoka Rombo kwenye Kenya kufanya biashara.
"Si unajua toka Rombo kwenda Kenya ni karibu sana, kipindi kile vijana wengi walikuwa wanakwenda Kenya kufanya biashara, hivi sasa hali imebadilika vijana wengi wanatoka kenya kuja Tanzania kufanya biashara." alisema Belinda.
Anadai kwa vile sanaa ipo katika damu yake alivyokuja Dar es Salaam aliamua kujifunza kuandika script na kuhakiki, miongoni mwa sinema ambazo alihakiki ni pamoja na Uwanja wa dhambi,  I love you, Bunge la wachawi,  Picnic, Popobawa, Zindiko na sinema mpya ya Bekitatu.
"Kwa vile nilikuwa na kipaji cha kuigiza  nilijikuta nikikosa kila wakati ninapoangalia sinema,  nikaamua kujinga katika kikundi cha Alwatan Artstis Theatre kilichokuwa chini ya uongozi wa  mwalimu wangu wa script, Haji Dilunga.", alisema Belinda
Baada ya kujiunga na kikundi hicho alishiriki kucheza sinema inayoitwa Julio na Romeo iliyotungwa na kuandikwa script na Haji Dilunga, katika sinema hiyo alicheza kama dada anayesambaratisha penzi la mdogo wake kwa kumtafutia msichana mwingine.
 Mbali ya sinema hiyo, alipata nafasi ya kushiriki katika sinema nyingine iliyotungwa na kuandikwa script na Haji Dilunga, inayoitwa Sound of soul.
Katika hali ya kuleta ushindani na changamoto katika ufanisi, Dilunga aliamua kuanzisha kundi la jingine linaloitwa Sun Shine Artists Theatre kwa ajili ya kuleta ushindani miongoni mwetu. Kwa bahati nzuri nilijikuta nikiwa katika Sun shine badala ya Alwatan, waigizaji wengine niliocheza nao sinema hizo nilizotaja wamebaki katika kundi la Alwatan.
Maisha ya kifamilia nimeolewa, nina watoto wawili wa kiume. Nampende mume wangu na kuheshimu, mwigizaji anayenivutia ni kutoka Nigeria anaitwa Omotola Jalade Ekeinde .  Anavutiwa na namna anavyoigiza na mapozi yake.
Belinda amewataka wapenzi na mashaki wanunue sinema ya Bekitatu wajionee kile alichofanya, watakubaliana naye kwa sanaa ni kipaji nasio kulazimisha kama wengine.
Amesema katika sinema ya Bekitatu amecheza kama mwanamke anayeishi na mfanayakazi wa ndani anayeitwa Sikitu au Bekitatu, katika sinema hiyo anaonekana anavyomtesa mfanyakazi wake wa ndani.
"Ni sinema nzuri inayosikitisha, kufurahisha na kuelimisha, kuikosa ni dhambi kubwa kwa sababu utakuwa umekosa ujumbe muhimu sana katika maisha yako,"alisema Belinda.Wale wanaotaka nakala ya sinema yetu wasikose kupiga namba hizi 0753 833773 au 0655 833 772.

Saturday, November 29, 2014

Sinema kumi za kitanzania zinazofanya vizuri sokoni

Mwaka huu kuanzia Januari mpaka Novemba zimeingia sokoni sinema nyingi sana,  kila sinema ilikuwa na utamu sambamba ubora wake, watayarishaji na waigizaji sambamba waongozaji walijitahidi kila mmoja kuhakikisha anafanya kazi nzuri itakayokubalika na jamii.
Kama tulivyosema mwanzo sokoni zimeingia sinema nyingi,  kati ya hizo  sinema kumi zimetokea kupendwa na watu wengi sana.  Tafiti za kupendwa  kwa sinema hizo zilizofanyika katika mkoa wa Dar es Salaam  na Arusha kwa wauzaji wa maduka ya jumla na  maduka ya rejareja,  sambamba na wauzaji wanaotembeza mitaani maarufu kwa jina la wamachinga.

 1.                                                       Jamila na pete ya ajabu
                                      Jamila imetokea kuvuwatia watoto wengi sana kwa mujibu wa
                                                   wadau wetu   waliotupatia taarifa hizo
                                                                   

                                                                                                                                                      
 2                                                                       Chausiku   

Chausiku imetokea kuwa gumzo kubwa katioka maeno ya uswahili
3                                                                Siri ya Giningi
                                                                             

                                                                                   
 4                                                             Zena na Betina
                                                                          
5                                                              Hakumu ya ndoa yangu
                                                                             
6                                                               Tom Boy  
                                                                       


 7                                                        Uliyemchokoza kaja
                                                                           



 

8                                                                    Nahama

                                                                           

 9                               Nendeze Mwali wa Kizaramo ( Sinema hii haina kava)

                                                                         

10                                                         Kwanini Mama 
                                                                        

                                                                     



Friday, November 28, 2014

Waigizaji vibonge wa Nigeria wanavyotesa na ubonge wao kuliko wembamba


Wakati  nigeria wasanii wa kike wenye maumbo makubwa na yakuvutia wanaongoza katika kurasa za mbele za magazeti ya udaku na majarida mbali mbali ya burudani sambamba na mitandao ya kijamii kutokana mavazi yao.  Mara nyinyi wasanii wanakuwa wanalipuka pamba za ukweli zinazoonyesha baadhi ya maungo yao yakiwa nusu. Kitendo hicho kimetokea kuwa gumzo kubwa katika miji  mbali mbali ya  nchi hiyo ,  miongoni mwa nguo wanazopenda kuvaa ni zile zinazoonyesha sehemu kubwa ya amatiti yao yakiwa wazi sambamba na mapaja yao. Wengine wanafikia mpaka kuonyesha vitovu vyao. Kwa mujibu wa  maelezo kwa nyakati tofauti wamesema si kitu cha ajabu kufanya hivyo kwani kila mmoja ana utaratibu wake wa kuvaa hasa kwenye matukio  mbali mbali cha muhimu ni kwamba hawatembei uchi wa mnyama. Kama kuna watu wanachukizwa au waandishi wanafuatilia maisha yetu, watajijua wenyewe kila ana stahili ya amaisha yake aliyochagua kuishi. Wafuatao ni miongoni mwa mastaa wanaotingisha kwa kuvaa mavazi yanawachanganya wanaume na hata wanawake wenzao, sambamba na kulalamikiwa na baadhi ya watu.
                                                                          
                                                                Ifeoma Okeke
Ni mwanamke anayejua  kuvaa kulingana na mwili wake unataka kuvalishwa nini, sio kujivalia ovyo ovyo kwa kuiga. Licha aya unene wa umbo lake bado anamvuto wa hali ya juu kutokana kupangili amvazi yake. Licha ya kuvaa nusu uchi bado anaonekana kutingisha kuvutia wanaume wengi kumtazama mara wanapobishana . Staa huyu alitamba na sinema ya Evil Genius, hata mara kwa mara amekuwa amesema hajisikii vibaya kwa jinsi anavyovaa na wala haoni ajabu au aibu. Mwanamama anakaribia kufikisha kilo mia mbili.


 
                                                                         

                                                         Chioma Toplis
                                                            
Ni mwanadada mwenye mvuto wa hali ya juu hasa namna anavyojua kumechisha mavazi yake viatu, licha kuwa bonge la mtu ni mpenzi wa viatu virefu.  Kwa mujibu wa maelezo amejikagua na kugundua  kama miezi ya karibuni uzito umekuwa ukipanda kwa kasi mpaka anashangaa. hata hivyo amesema licha kufanya maoezi bado uzito unaongezeka, ametamba na sinema ya Stolen Bible



                                                                     Eniola Badmus
Ana bonge la kitambi siku hizi na wala hajawahi kusikika akilalamika. Msanii huyo maarufu kwa jina la Gbogbo Big Girl, ni binti anayependa kujipodoa ingawa hakuna uhakika kama anajua madhara yake. Uchunguzi unaonyesha kwamba mwili wake mkubwa ndiyo umemfanya akawa maarufu zaidi kuliko kazi anazofanya.




                                                                            


                                                                    Adaora Ukoh
                                                                  
Marafiki zake wamesikika wakimuonya mara kadhaa, lakini ni kama vile anaona yuko sawa. Miezi michache iliyopita alizindua gauni kubwa alilolipa jina la Adaora akiwa anamaanisha kwamba ni nguo maalum kwa ajili ya wasichana mabonge kama yeye. Anaamini kila mwanamke ni mrembo na uzuri uko ndani na si ukubwa wa mwili japokuwa ameanza mazoezi ya gym.

                                                                                Foluka Daramola                                                                                     
Foluke Daramola anaijua kazi yake, acha apewe sifa. Lakini mashabiki wake wamekuwa wakiguna kila wanapomuona kutokana na unene wake mkubwa. "Unene au mwili wa mtu ni suala binafsi la maisha ya msichana hakuna wa kumuamulia, najua ninachopaswa kufanya," ndivyo anavyosema.

Kidawa ni sinema yenye mazingira ya uswahili kikweli kweli

                                                  Nuru Mohamed a.k.a Kidawa
                                                                Mohamed Nurdin
                                                      Haji Adam  na Mohamed Nurdin
                                                               Haji Adam
                                                              Zainabu Mshindo

Katika makala yetu ya Sinema , leo naiangalia Sinema  inayoitwa Kidawa Uswahilini. Iliyotayarishwa na kampuni ya  Kapelele ya jijini Dar es Salaam na kusambazwa na kampuni ya BMO, pia  ya jijini Dar es Salaam. Ni filamu nzuri inayoelezea  vituko na visa vya wakazi wa maeneo ya uswahilini, hasa wale wanaoishi katika nyumba za kupanga.
Kidawa uswahilini inamzungumzia mwanamke anayeitwa Nuru Mohamed aliyecheza kwa jina la Kidawa na rafiki yake  Zainabu Mshindo aliyecheza kwa jina la Cecy ,  Mohamed Nurdin aliyecheza kwa jina Faiza, Haji Adam aliyecheza kama Mwasa pamoja na wapangaji wengine.
Hadithi (Story):
Wazo la hadithi  lilikuwa zuri sana, liliangalia mazingira ya maisha ya kweli wa wakazi wa maeneo ya uswahili na vituko vyao. Umbeya, chuki, shida, wivu wa kimaendeleo, ugomvi, matusi, kusutana, vyote hivyo vilionekana katika hadithi hii.  Kitu ambacho kwa watu wanaoishi maeneo ya watu wenye uwezo ni nadra kushuhudia mambo kama hayo. 
Nuru au Kidawa amecheza kama mwanamke mkorofi anayegombana na wenzake kila wakati,  nyumba inakosa amani na furaha kutokana na tabia yake ya ukorofi.  Zainabu au Cecy  katika sinema hiyo amecheza kama  rafiki wa Kidawa, anayevutiwa na ukorofi anaofanya Kidawa.
Mashoga hao wawili wametokea kuwa kero kwa wapangaji wenzao ambao ni Haji Adam au Mwasa na  Mohamed Nurdini au Faiza pamoja na wapangaji wengine wanaoishi katika nyumba hiyo yenye idadi kubwa ya wapangaji.
Sinema inaanza kwa Kidawa kupigana na mpangaji mwenzake anayeitwa Mwajuma,  majirani wanajitokeza kuwatenganisha,  kidawa anaonekana kutokubali na kuendelea kutoa matusi. wakati hilo likiwa bado halijapatiwa ufumbuzi, Mickynessy Joseph  aliyecheza kwa jina la Sinai  anamkuta Kidawa na rafiki yake Cecy wanamsema dada yake anayeitwa Sina. Wanarushiana maneno machache yanayoashiria kutaka kuleta ugomvi.
Kabla ya kumalizika hilo, wapangaji wote wanakaa kikao kujadili suala la umeme, kabla ya kufikia mwaka wa kikao hicho. Kidawa anakivuruga kikao kwa maneno yake ya kashfa na matusi na kisha kuondoka zake,  akidai kwamba hawezi kuendeshwa na watoto.
Kidawa aliongea hivyo baada ya watoto waliokuwa katika kikao hicho kudai kwamba Kidawa na Jenga wanamatumizi mabaya ya umeme.  Jenga ana mafriji mawili, Kidawa anapitisha marundo ya nguo ya rafiki zake kupiga pasi.
Kauli hiyo inamchukiza Kidawa na kuondoka zake katika kikao hicho, rafiki yake Cecy ananyanyuka anamfuata huku akiwa anatoa maneno ya matusi kumwambia miongoni mwa watoto waliokuwa wakichangia katika kikao hicho. Kiujumla  sinema hiyo inaelimisha na kuburudisha.
Usaili (Casting )
Mtu aliyefanya usaili (Casting Director)  alifanikiwa kuchagua waigizaji waliofanikiwa kuzitendea haki nafasi zao walizopangiwa kucheza.  Kila mmoja amecheza kwa kiwango cha hali ya juu, pongezi kwa casting director kwa kazi nzuri aliyofanya.
Mavazi (Costumes)
Aliyepangwa kuhakikisha waigizaji  wanavaa nguo zinazoendena na wakazi wa mitaa ya uswahilini,  kila mwigizaji alivaa kulingana na nafasi yake aliyocheza. Wapo wale waliovaa na  na kuonekana ni miongoni mwa wenye maisha nafuu zaidi ya wenzao kama vile Sinai na dada yake Sina anayeishi na mume wa mtu anayeitwa Faiza ambaye ni Nurdini. Wengine walionekana  ni wale wenye maisha ya kawaida hata Televishana hawana wanaangalia katika vyumba vya wenzao.
Mapambo (Makeup)
Mtu wa mapambo alifanikiwa kuwapamba vizuri na kuonekana ni miongoni mwa waliofanikiwa kuvaa taswira ya wakazi wa mitaa ya uswahilini kwa namna walivyopambwa na kupambika.
Mandhari(Location)
Mtu aliyepewa jukumu la kutafuta mandhari (Location) alifanikiwa kutafuta nyumba yenye uwezo wa kuchukua wapangaji wengi kwa wakati mmoja. Ki kweli kabisa anastahili pongezi kwa kufanikiwa kutafuta nyumba inayochukua wapangaji wengi kama nyumba hiyo iliyotumiwa kuchezea sinema ya Kidawa uswahiini.
Mwanga: (Light)
Mshika taa aliweza kushirikiana  vizuri na camera man wake  kuhakikisha wanatoa picha zenye ubora mzuri, licha baadhi ya scene zilionekana kuwa na mwanga hafifu pamoja na ubora mdogo. Alipoulizwa camera man   anayejulikana kwa jina la Rajabu Ngatale aliyeshuti sinema hiyo alisema baadhi ya scene zilitoka hivyo kutokana na camera ya mwanzo waliyotumia ilikuwa ina matatizo ya kiufundi.
Sauti (Sound man)
Sauti katika sinema hii haikuwa nzuri  sana,  hasa zile scene za  nje zilikuwa zina mvumo wa upepo. katika scene za ndani kutlikuwa na tofauti kubwa ya mabadiliko ya sauti hasa inapoingia shot ya CU  yaani ya karibu sauti inasikika vizuri. Inapokuja shot ya mbali yaani Long shot sauti inakuwa ndogo.  Tatizo lilitakiwa kuwekwa sawa na mhariri aliyehariri sinema hiyo.
Mhariri (Editor)
Mhariri alijitahidi kadri ya uwezo wake, lakini alishindwa  kuweka sawa tatizo la sauti. wakati mwingine mhariri anatakiwa  kuwa makini na sauti, sinema bila ya kuwa ana sauti inayosikika vizuri inapoteza utamu wake hata kama itakuwa stori  nzuri.
Muongozaji (Director)
Katika sinema muongozaji ni mtu muhimu sana katika kuhakikisha sinema inatayarishwa katika ubora unaotakikana kulingana na hadithi husika kwa kulinda wazo la mwandishi au mtunzi, ukiangalia filamu hii script imetendewa  haki licha ya mapungufu madogo madogo yalijitokeza kutokana  na sababu za kiufundi. Kwa wasiobahatika kuiona waitafute kushuhudia ufundi wa waigizaji wa sinema hiyo. Kwa naishi hapa tukutane katika sinema nyingine ya wiki..

Wema bado ni kipenzi cha wabongo kila anachofanya wanashabikia

                                                                        
                                                      
Bila ya kupindisha ukweli mwigizaji Wema Sepetu ni miongoni mwa waigizaji wenye nyota kali sana kwa wapenzi na mashabiki,  ukitaka kudhibitisha hilo angalia magazeti ya udaku yakiwa na picha yake sambamba na stori yake. watu wengi kwenye daladala utawaona wanamagazeti hayo wanasoma. Udhibitisho mwingine angalia idadi ya wasomaji na watazamaji wa video zinazomuhusu yeye  katika blog mbali mbali ni kubwa kuliko waigizaji wengine.  Udhibitisho mwingine jaribu kuchungu wale watu waliokuwa karibu yake walivyojipatia umaarufu kubwa, baada ya kuachana nao wengi wao wanapoteza umaarufu.  Kama unataka kuwa maarufu jipendekeze kwa  Wema hata kwa kubeba mkoba wake au kumfuta jasho, siku tatu ya kuwa naye tayari utapamba katika kurasa za magazeti ya udaku. Wema bado ni kipenzi cha wabongo, habari ndiyo.

Toni Braxton kuigiza kama msagaji

         




Mkali wa  muziki wa taratibu Toni Braxton ameonyesha nia aya kujitumbukiza katika fani ya uigizaji, baada  ya mwaka jana kutangaza kustaafu mambo ya muziki kama sio kupumzika.  Amesema nafsi yake inamtuma kufanya kitu ambacho alikuwa anakipenda sana toka zamani.Kwa mujibu wa maelezo yake anataka kuigiza sinema, tena anataka kuigiza kama msagaji. "Toka zamani nilikuwa na nndoto ya kuigiza kama mwanamke msagaji, nadhani sasa ndoto yangu inaweza kutimia kwa kufanya kitu roho inapenda." aliema Toni Braxton mwenye miaka 46, amabye amewahi kunyakuwa tuzo nne za grammy.











Thursday, July 18, 2013

Danny Schechter ameitangaza Tanzania kwenye Movie ya Mandela

                                                                              
                                                                     Danny Schechter
Danny Schechter  a.k.a The News Dissector kwa wale wasio mfahamu ni mtayarishaji  kama sio mtengenezaji wa sinema ya Nelson Mandela – “Countdown to Freedom” na “Mandela in America” ametaka dunia kuiheshimu Tanzania kwa nafasi yake kubwa kwenye kutengeneza demokrasia Afrika Kusini.
Schechter anayefanya dokumentari ya utengenezaji wa filamu ya Long Walk to Freedom kama alivyotakiwa na Nelson Mandela mwenyewe, alisema Tanzania ilitoa ushirikiano mkubwa kukomboa mataifa mengi ya Afrika ikiwemo Afrika Kusini.
Jumapili katika Tamasha la ZIFF ilikuwa ni siku ya kuangalia Afrika Kusini kabla na baada ya Uhuru. ZIFF iliweka siku maalumu ya Afrika Kusini kutokana na maendeleo ya hali ya afya ya Nelson Mandela ambayo sasa inazungumzwa duniani kote.
Mandela ambaye katika dokumentari hiyo anaonekana akifafanua vitu mbalimbali, alielezwa na Schechter kama mtu maarufu ambaye hakutaka kuitwa mtakatifu pamoja na kwamba aliombwa kutengenezewa sanamu na kuwataka wasifanye hivyo na badala yake kusaidia ujenzi wa zahanati.
Alisema dunia inapaswa kutambua kwamba katika ukombozi wa Afrika Kusini, Tanzania ni nchi muhimu ingawa dunia inaonekana kutotambua hilo lakini wenyewe wa Afrika Kusini wanafahamu.
Alisema baada ya kuwapo na nia ya kutengeneza filamu yake, Madiba alimwandikia barua ya kumtaka kutengeneza dokumentari inayohusu utengenezaji huo kwa kuhakikisha ukweli uliopo kama unazingatiwa.
Alisema hali hiyo ilimfanya kufika Tanzania japo alishawahi kufika wakati wa harakati za ukombozi. Schechte ambaye ni mwandishi wa habari za uchunguzi, mtengeneza sinema huru, bloga na mhakiki vyombo vya habari, alisema ni vyema dunia ikatambua mchango wa Tanzania kwa ukombozi si wa Afrika Kusini, bali na mataifa mengine ya Afrika.
Alisema pamoja na utawala wa Makaburu kuzishambulia nchi zilizokuwa zinasaidia ANC kama Zimbabwe, Msumbiji, Angola na Zambia, ilishindwa kufanya hivyo kwa Tanzania ambayo licha ya kuwa na makambi ya mazoezi ya kivita, pia ilikuwa na shule za kufunza viongozi wa baadaye wa Afrika Kusini, Morogoro.
Dukumentari hiyo yenye tofauti kubwa na zile zinaozotengenezwa kwa ajili ya kuoneshwa katika televisheni, inamweleza Mandela kama mtu wa watu huku waliohojiwa wakielezea matumaini na nini kinafanyika.

Sunday, July 14, 2013

Demi More kuacha kuigiza sinema

                                                                          Demi More
 Mwigizaji maarufu duninia mwanadada Demi More anafikiria kuacha kuigiza na kufanya kazi ya kufundisha mazoezi ya ya viungo maarufu kama yoga. Demi amefikia hatua hiyo baada ya kupigwa talaka na aliyekuwa mume wake.
Mwanadada huyo alipigwa talaka baada ya kukubali mwenye bila ya kulazimishwa kama alikuwa na tabia ya  kutoka nje ya ndoa yake.


Sinema yangu ya Safari itachukua Tuzo- Richie

                                                                    
                                                                  Single Mtambalike
Nyota wa sinema za kitanzania, mkongwe Single Mtambalike maarufu kama Richie ametamba kuchukua tuzo kupitia sinema yake mpya ya Safari.
"Nimetayarisha sinema ya Safari kwa umakini, hivyo ni lazima iwe filamu ya kuingia katika tuzo mwaka huu kulingana na ubora wake, hata wasanii walioigiza wameigiza kwa kiwango cha juu," alitamba Richie.
Mkongwe huyo anadai kuwa yeye ni bora kwani ndiye msanii wa kwanza kabisa Tanzania kupewa tuzo na M-net mwaka 2006 huku akisifia utaratibu uliotumika kupatikana mshindi katika tuzo hizo.