Showing posts with label Kuigiza. Show all posts
Showing posts with label Kuigiza. Show all posts
Friday, November 28, 2014
Toni Braxton kuigiza kama msagaji
Mkali wa muziki wa taratibu Toni Braxton ameonyesha nia aya kujitumbukiza katika fani ya uigizaji, baada ya mwaka jana kutangaza kustaafu mambo ya muziki kama sio kupumzika. Amesema nafsi yake inamtuma kufanya kitu ambacho alikuwa anakipenda sana toka zamani.Kwa mujibu wa maelezo yake anataka kuigiza sinema, tena anataka kuigiza kama msagaji. "Toka zamani nilikuwa na nndoto ya kuigiza kama mwanamke msagaji, nadhani sasa ndoto yangu inaweza kutimia kwa kufanya kitu roho inapenda." aliema Toni Braxton mwenye miaka 46, amabye amewahi kunyakuwa tuzo nne za grammy.
Mkenya Lupita Nyong'o kuigiza katika Americanah
Muigizaji nyota kutoka Kenya Lupita Nyong'o amejumuishwa katika wasanii watakaoigiza katika filamu ya AMERICANAH inayotokana na kitabu cha mwandishi Chimamanda Ngozi Adichie. Filamu hiyo haitofautini sana na ile sinema ya ''12 Years a Slave'' iliyompelekea mrembo huyo kushinda tuzo la Oscars mwezi Februari itatayarishwa na kampuni ya PLAN B P inayomilikiwa na Mtayarishaji na muigizaji maarufu wa filamu, Brad Pitt . Filamu hiyo mpya ya AMERICANAH inaelezea mada ya mapenzi kati ya wapenzi wawili wa Nigeria ambao licha ya penzi kuchanuka kati yao wanatenganishwa na maswala ya uhamiaji. Muigizaji huyo aliwaambia mashabiki wake kuwa ni heshma kubwa kwake kupewa nafasi ya kuigiza katika filamu hiyo inayotokana na kitabu cha Adichie. Kitabu hicho cha Americanah, kiachoelezea maisha ya wapenzi wawili Ifemelu na Obinze. Kitabu hicho kilishinda tuzo la ''US National Book Critics Circle Award mwaka uliyopita. Aidha kimeteuliwa kuwa moja kati ya vitabu kumi bora na jopo la 'The New York Times Book Review. Nyongo aliiambia BBC kuwa baada ya kukisoma kitabu hicho , alitamanishwa na jinsi Ifemelu na mpenzi wake Obinze,walivyostahimili majaribu mengi katika uhusiano wao . Hali ambayo inawakumba waafrika wengi ambao kutokana na tamaa ya mafanikio wanakwenda ughaibuni kutafuta ajira na wengine kwa masomo ya juu. Mbali na Americanah , Adichie anajivunia tunu ya uandishi wa vitabu vingine kama vile Purple Hibiscus na Half of a Yellow Sun, ambayo pia imefasiriwa na kuigwa katika filamu na muigizaji nyota katika 12 Years a Slave , Chiwetel Ejiofor. Nyong'o aliwavutia wapenzi wa filamu kote duniani aliposhirikiana na Ejiofor na kutwaa taji la Oscar katika 12 years a slave.
Sunday, July 14, 2013
Beckham kuigiza nafasi ya James Bond
David Beckham
London, England
Mke wa aliyekuwa mwanasoka wa Klabu ya Manchester United, Victoria Beckham amependekeza jina la mumewe, David Beckham kuwa miongoni mwa majina yatakayochaguliwa kupata nafasi ya kuigiza kama James Bond katika mfululizo wa sinema za 007, zinazomtumia muhusika mkuu anayeitwa James Bond.
Mapendezo hayo yanafanyika baada ya mwigizaji, Daniel Craig anayecheza sasa kama James Bond kubwaga manyanga. Majina yaliyopendekezwa ni kucheza kama James Bond ni pamoja na Christian Bale, Henry Cavill, Tom Hardy na Idris Elba.
Victoria ana amini Beckham anaweza kuitendea haki nafasi hiyo kuliko wote waliotaja kuziba pengo la Daniel Craig anayeacha kucheza nafasi hiyo.
" Nina uhakika Beckham ni bidhaa inayouzika, kama watamtumia kucheza kama James Bond. Sinema hayo itapendwa na watu wengi sana hata wale ambao sio mashabiki wa kuangalia sinema, kwa sababu Beckham ni mtu wa watu," alisisitiza Victoria alipokuwa anaongea.
Kama watampa nafasi ya kucheza kama James Bond, Beckham atafanya vizuri, kwanza ni mwanaume mwenye mvuto. Sura yake nzuri na shepu ya umbo lake ni nzuri tofauti na wanaume. Kwa hiyo watu watapenda kumtazama.
Hata hivyo Beckham mwenyewe alipoulizwa, alisema hana uhakika kama ataweza kufanya vizuri, kwa sababu hajawahi kuigiza au kusimama mbele ya camera kuigiza.
"Sina uhakika kama nitakuwa mzuri katika kuigiza, kwa sababu sijawahi kufanya kitu kama hicho katika maisha yangu. Ila kama nitapewa nafasi naweza kufanya. Nina rafiki yangu Tom Cruise ambaye ni mwigizaji mkubwa, labda ninaweza kuwa kama yeye. Ila sijafikiria kitu kama hicho kwa sasa," alisema Beckham, wengi wanamkumbuka kwa uhodari wake uwanjani.
Demi More kuacha kuigiza sinema
Demi More
Mwigizaji maarufu duninia mwanadada Demi More anafikiria kuacha kuigiza na kufanya kazi ya kufundisha mazoezi ya ya viungo maarufu kama yoga. Demi amefikia hatua hiyo baada ya kupigwa talaka na aliyekuwa mume wake.
Mwanadada huyo alipigwa talaka baada ya kukubali mwenye bila ya kulazimishwa kama alikuwa na tabia ya kutoka nje ya ndoa yake.
Mwigizaji maarufu duninia mwanadada Demi More anafikiria kuacha kuigiza na kufanya kazi ya kufundisha mazoezi ya ya viungo maarufu kama yoga. Demi amefikia hatua hiyo baada ya kupigwa talaka na aliyekuwa mume wake.
Mwanadada huyo alipigwa talaka baada ya kukubali mwenye bila ya kulazimishwa kama alikuwa na tabia ya kutoka nje ya ndoa yake.
Subscribe to:
Posts (Atom)













