Friday, November 28, 2014

Mkenya Lupita Nyong'o kuigiza katika Americanah

 







Muigizaji nyota kutoka Kenya Lupita Nyong'o amejumuishwa katika wasanii watakaoigiza katika filamu ya AMERICANAH  inayotokana na kitabu cha mwandishi Chimamanda Ngozi Adichie. Filamu hiyo haitofautini sana na  ile sinema  ya ''12 Years a Slave'' iliyompelekea mrembo  huyo kushinda tuzo la Oscars mwezi Februari itatayarishwa  na kampuni ya PLAN B P inayomilikiwa na Mtayarishaji na muigizaji  maarufu wa filamu, Brad Pitt . Filamu hiyo mpya ya AMERICANAH inaelezea mada ya mapenzi kati ya  wapenzi  wawili wa Nigeria ambao licha ya penzi kuchanuka kati yao wanatenganishwa na maswala ya uhamiaji. Muigizaji huyo aliwaambia mashabiki wake kuwa ni heshma kubwa kwake kupewa nafasi ya kuigiza katika filamu hiyo inayotokana na kitabu cha Adichie. Kitabu hicho cha Americanah, kiachoelezea maisha ya wapenzi wawili Ifemelu na Obinze. Kitabu hicho kilishinda tuzo la ''US National Book Critics Circle Award mwaka uliyopita. Aidha kimeteuliwa kuwa moja kati ya vitabu kumi bora na jopo la 'The New York Times Book Review. Nyongo aliiambia BBC kuwa baada ya kukisoma kitabu hicho , alitamanishwa na jinsi Ifemelu na mpenzi wake Obinze,walivyostahimili majaribu mengi katika uhusiano wao . Hali ambayo inawakumba waafrika wengi ambao kutokana na tamaa ya mafanikio wanakwenda ughaibuni kutafuta ajira na wengine kwa masomo ya juu. Mbali na Americanah , Adichie anajivunia tunu ya uandishi wa vitabu vingine kama vile Purple Hibiscus na Half of a Yellow Sun, ambayo pia imefasiriwa na kuigwa katika filamu na muigizaji nyota katika 12 Years a Slave , Chiwetel Ejiofor. Nyong'o aliwavutia wapenzi wa filamu kote duniani aliposhirikiana na Ejiofor na kutwaa taji la Oscar katika 12 years a slave.
















No comments:

Post a Comment