Friday, February 15, 2013

Anna Michael utakumbukwa daima kwenye Movie bongo, Tanzania




                                            Marehemu Anna Michael enzi ya uhai wake                                 
Jina kama Sina alilotambanalo katika kikundi cha Kidedea au Tunu alilovuma nalo katika sinema ya I love you,ni kilelezo tosha  kama uwezo wa Anna Michael katika sanaa ya kuigiza ulikuwa wa kiwango cha juu.

Majina hayo yalitaka kufuta jina lake halisi la Anna Michael, alilopewa na wazazi wake. Wahenga walisema kila kilichokuwa kizuri hakidumu sana, ni kauli inayowakilisha ukweli wa machungu yanayouma. Lakini yote ni mipango ya mwenyezi mungu.

Licha ya wazazi wake, mtoto wake, ndugu, marafiki, waigizaji wenzake, wapenzi na mashabiki wake walimpenda, lakini mungu alimpenda zaidi na kumchukua.

Ni miaka minne sasa tangu Anna Michael hatutoke kimwili na kiroho lakini kazi zake zitaendelea kuwepo katika maisha yetu ya kila siku.

Kila utakapotazama sinema ya Uwanja wa dhambi, I love you, Picnic na Confess. Utaweza kujionea kipaji alichobahatika kuwa nacho marehemu.

Wasanii wanaochipukia wangetafuta sinema alizocheza waweze kujifunza mambo muhimu.

Marehemu alikuwa anavaa taswira anayotakiwa kucheza, ni vigumu kwa sasa kupata wasanii wenye uwezo huo. Wengi wanapoteza uhalisi wanapoigiza.

Kuna wale wanaopoteza uhalisi wa sauti, muonekana na hata mavazi. Kazi kwenu wasanii chipukizi. 

Monday, February 11, 2013

Mavazi yanayotumika yanaondoa uhalisi wa sinema Tanzania



Imebainika kama watazamaji wengi wa sinema hasa wabongo wanavutiwa na mavazi ya waigizaji. Uchunguzi uliofanywa umefanikiwa kugundua kama watazamaji wa kiume wanavutiwa zaidi ya mavazi ya waigizaji wa kike, hasa wanapokuwa katika scene inayowaonyesha wamevaa night dress.

Wanaume wengi wanadai night dress zinawapendeza wanawake, Zinawachochea na kuamsha hisia zilizolala. Mavazi mengine yanayowavutia ni vimi, yaani vile vimini vifupi sana kuvuka magoti, Sambamba na zile nguo za kubana zinazoonyesha shepu zao.

Wanaume wengine wanavutiwa na aina ya viatu wanavyovaa waigizaji wa kike, wengi wanapenda kumuona muigizaji amevaa viatu virefu kama vile 6inch stiletto high heels, high heels Pumps, high heels Platform, Wedge heels, Metal Spike high heels, Boots high heels and high heels Sandals.

Kwa upande wa wanawake wanavutika na mitindo wanayovaa waigizaji wa kike, wapo wanaongalia mitindo ya nguo, nywele na viatu. Wengine wanakwenda mbali sana na kujikuta wakivutiwa na aina ya uongeaji na hata mapozi ya msanii.

Kwa kuzingatia hilo, ndiyo maana sinema nyingi za kibongo zinapoteza uhalisi kwa ajili ya kutaka kuwafurahisha wapenzi wao.

Utakuta msichana anacheza nafasi ya kijijini, amevaa mavazi ya kimjini. Au msichana anacheza kama sekretari amevaa kimini. Au msichana anaonekana yupo nyumbani amevaa kiatu kirefu. Kwa ufupi uhalisi wa sinema za kitanzania unapotea kwa kuendekeza ujinga.


Soko la Sinema za kinaigeria la shuka nchini, Tanzania

 
                 Mastaa wa sinema za kinaigeria katika picha ya pamoja Waigizaji wa Nigeria
 
                                                                        Mastaa wa Kinageria       
Kabla ya soko la sinema za kitanzania kupata umaarufu, sinema za kinaigeria zilikuwa na mvuto mkubwa sana nchini, hivi sasa zimepoteza umaarufu wake. Watanzania wengi wamezinduka na kuanza kupenda sinema zinazotayarishwa nchini na waigizaji wa kitanzania. Japokuwa sinema za kitanzania zinamapungufu mengi, bado watanzania wanazipenda.

Kinachotakiwa kufanywa na watayarishaji wa sinema ni  kuwa makini wanapoanza kutayarisha. Ili kukwepa makosa ya kijinga ambayo hayahitaji elimu ya chuo kikuu kuweza kuyabaini.

Watayarishaji, waigizaji, waongozaji, waandishi wa script sambamba na wadau wa sinema wasipokuwa makini. Wanaweza kusababisha sinema za nje ya Tanzania kama vile wanaigeria, waghana na waafrika kusini kurudi katika chat ya juu.Kama ikitokea hivyo soko la sinema la kitanzania litapotea kama sio kusambarataika kabisa.

Actress Mwajuma anatamba kwenye redio Dar es Salaam, Tanzania.

 
                      Mwajuma aka Maimuna akiwa juu ya kaburi  katika sinema ya uwanja wa dhambi
Mwajuma  Abdul a.k.a Maimuna  ni  muigizaji ambaye huwezi kumaliza siku nzima bila ya kusikia sauti yake kwenye tangazo lolote redioni.  Kwa wale wanaofahamu sauti yake watakuwa mashahidi  wa hiki kilichoandikwa hapa.

Baadhi ya matangazo yake ni pamoja na lile la bidhaa bora za Azam, Ulevi noma, Nimeshinda  na Airtel, Airtel money linalosema nimetumia elfu ya kumi ya kununua dawa, nimefika dukani nimekuta dawa inauzwa elfu kumi hiyo hiyo na mengine mengi.

Mbali ya kushiriki matangazo ameshiriki kuigiza katika sinema mbali mbali kama vile Lazima ufe Joram, Uwanja wa Dhambi, I love you, Picnic, Bunge la wachawi, Popobawa, Zindiko na Bayana  zinapatikana madukani. Sinema ya Confess na Julio na Romeo inatarajia kutoka hivi karibuni.

Nurati ndani ya movie ya Julio na Romeo Tanzania


Kikundi cha Alwatan Artist Theater kimemtambulisha muigizaji mpya anayeitwa Nurati Ngereshi katika sinema yake ya Julio na Romeo inayotarajia kuingia sokoni hivi karibuni.

Kabla ya kuanza kuigiza, Nurati alikuwa akihakiki script za kundi hilo, lenye makao yake makuu Ilala Kimako. Sinema zote za kundi hilo utakutana na jina lake kwenye nafasi ya script editor.

Kwa vile stori ya Julio na Romeo lilikuwa ni wazo lake, alilomsimulia mwandishi wa script, baada ya kuandikwa alishauriwa kucheza

Katika sinema hiyo ameshiriki kama msichana anayempinga mdogo wake wa kiume anayeitwa Julio kumuoa msichana anayeitwa Romeo.

Wakati huo huo alikuwa akimshawishi rafiki yake Tunda aliyerejea nchini toka Marekani kuolewa na mdogo wake Julio. Ni sinema nzuri yenye mafunzo kwa jamii, inaweza kuangaliwa na watu wa rika zote.

Stella ni zao la Alwatan Artist Theater Tanzania



Stella Baltazar


Msanii anayenyemelea kuwa mkongwe katika fani ya sinema, Stella Baltazar ni zao la kikundi cha Alwatan Artist Theater.

Stella aliletwa kampuni ya Heko Production na Marehemu Salum Karanda kwa la kucheza sinema inayoitwa Mikono mwa nunda, wakati huo alikuwa hajawahi kushiriki kikundi chochote cha sanaa.

Kwa vile Stella alikuwa na vitu vitano ambayo A, B, C, D, E. kwa ufanunuzi ni kwamba A for appearance, B for body structure, C for civilization, D for discipline na E for education, alipatia nafasi ya kucheza kama Nunda, msichana anayeua watu na kujidai ni Nunda mla watu.

Kwa bahati mbaya sinema hiyo haikuweza kutayarishwa. Mzee Karanda alimchukua tena na kumfikisha kikundi cha Alwatan, Uongozi wa kikundi ulimpokea na kumfundisha mbinu mbali mbali za kuigiza

Sinema yake ya kwanza ilikuwa Uwanja wa Dhambi aliyocheza kwa jina la Shubiri. Sinema ya pili ilikuwa I love you aliyocheza kwa jina la Sophia.

Baada ya hapo aliamua kujiunga na kikundi cha Shirikisho kilichokuwa kinarusha tamthilia yake televisheni ya ITV.
Katika tamthilia hiyo alikuwa akitumia jina la Kitalansi, baadaye alijikuta akipata nafasi ya kushiriki sinema zilizotayarishwa na kampuni ya Game first Quality Tanzania. Huko alicheza sinema nyingi kama vile Red Valentine na nyingine nyingi.






Sinema Tanzania, Inakuwaje movie zake kuwa na majina ya kizungu


Wapenzi na mashabiki waliobahatika kuongea na mtandao wa Swahili Cinema News, wamesema sinema za kitanzania kuwa na majina ya kizungu, ni ushamba na ulimbukeni wa hali ya juu.

“ Binafsi yangu sijawahi kuona sinema ya kihindi yenye jina la kizungu, au sinema ya kichina, Kijapan na kiarabu  zenye majina ya kizungu. Kama zipo itakuwa na jina la kizungu na jina la lugha yao" alisema Joshua Daniel.

Bi Sauda Ramadhani amesema sinema zilizotoka mwanzo zilikuwa nzuri, zilizingatia maadili ya kitanzania kuanzia stori, uvaaji, uchezaji na jina la sinema kuwa katika lugha ya kiswahili.

Alizitaja sinema hizo ni Nsyuka, Fungu la kukosa, Ngome ya Mwanamalundi, Lazima ufe Joram, Mambo ya ngoswe na nyingine nyingi za wakati huo.

“ Baada ya kuingia watayarishaji wanaopenda kuona mapaja ya watoto wetu wa kike, wakabadili mfumo wa utengenezaji sinema kwa kuandika majina ya kizungu.Kuwavisha nguo za ajabu mabinti wetu na kuwalazimisha kupigana mabusu, yaani huwezi kuangalia na watoto zako." Alisisitiza Bi Sauda.

Jaffar amesema kabla ya kina Ray, Tino, Johari, Mainda, Teya, Tito, Swebe, Maya, Zawadi, Nora, Nina na wengine, hawajaanza kuigiza sinema.

Walikuwa wakizingatia maadili katika michezo yao ya kwenye televisheni. Baada ya kuanza kujiunga na makampuni ya kutayarisha sinema, walibadilika kimaadili na kuanza kuvaa taswira ya kishetani. Taswira iliyowachukiza watazamaji wao.

“ Binafsi nilichukizwa na muonekano wao mpya, kwanza walikuwa wanaiga maadili ya kinaigeria kuanzia stori mpaka uchezaji." Alidai Jaffar.