Wednesday, January 28, 2015

Waigizaji wa kike Nigeria na vituko vyao

Wakati waigizaji wa Marekani na Ulaya wakiongoza kwa vituko vyao wanavyofanya kila kukicha, tayari  waigizaji wa Nigeria yaani Nollywood wamekumbwa na  kashfa kama sio vituko vya kujihusisha na picha za uchi.  Wengi wao wamekuwa wakipiga picha za nusu uchi  au uchi kabisa na kuzitupia katika mitandao ya kijamii.

                                                            
                                                    Mercy Johnson
Mercy Johnson alivuma hata kabla ya kuolewa na Prince Odi Okojie mwezi Agosti mwaka jana. Picha zake za uchi zilizagaa kwenye mitandao kadhaa na magazeti ya udaku. Harusi yake ndio ikavuma zaidi kwa madai kuwa alimpiku mwanamke mwingine ambaye alikuwa aolewe na Prince.
                            
                                                     Ini Edo
Hata yeye ameandamwa na kashfa za ngono, awali kabla hajaolewa, ilivumishwa kwamba alikuwa mchumba wa bosi mmoja wa majimbo ya kusini mwa Nigeria.  Kutokana na mwendo wake ndoa yake imevunjika. Hata anafurahi kuvunjika kwa ndoa yake.        
                                                                       

                                                              Tonto Dikeh
Kila mara yupo kwenye magazeti tangu mwaka 2006 alipoanza kuvuma. Leo utamsikia na kashfa ya ulevi, kesho kagombana na mtu. Kwenye mwili wake amechora tattoo 57 za aina mbalimbali. Ni mvutaji sigara mahiri na aliwahi hata kumkera Van Vicker wakati fulani kwa tabia hiyo, amekuwa akigombana ana wenzake kila mara.
                                                          

                                                     Iyabo Ojo

Alikuwa na bifu na msanii mwenzake, Lizzy Anjorin mpaka wakafikia hatua ya kutishiana kufanyiana uchawi , lakini wakapatanishwa na kigogo mmoja wa serikali. Habari zilizoripotiwa hivi karibuni ni kwamba alikutwa akifanya mambo ya ajabu na mwanaume mmoja kwenye gari jijini London na picha zikasambazwa.
                                                            

                                                Funke Akindele

Alivumishiwa mambo mengi sana, lakini kikubwa ni hivi karibuni iliporipotiwa kwamba ameolewa na kuwa mke wa tatu kwa mumewe. Lakini yeye hana matatizo na hilo.
                                                               
                                                            Genevieve Nnaji
Genny, kama anavyopenda kuitwa, amehusishwa kuwa na uhusiano na wasanii kama Ramsey Nouah, RMD na Pat Attah. Ni miongoni mwa wasanii wenye mambo mazito ya nyuma ya pazia ambayo hayawezi kusahaulika ikitajwa kwamba ni mlevi na mvutaji mahiri.
                                                              
                                                                          

                                                 Tayo Odueke (Sikiratu Sindodo)
Ametuhumiwa kuwa na uhusiano na vigogo wengi wa Serikali mpaka wengine wakampeleka nje kuhiji. Ingawa amekuwa akikanusha, lakini vituko vyake vya mara kwa mara vimemfanya asipotee kwenye uso wa jamii.
                                                                   

                                                        Stella Damasus
Alikuwa anachukuliwa kama msanii mtulivu, lakini madai kwamba amevunja ndoa ya staa mwenzake, Doris Simeon, yamemchafua.  Wawili hao wamekuwa wakikanusha, lakini ukaribu wao umeibua maswali mengi kama kweli ni biashara tu au kuna mengine?


                                                               Bukky Wright
Ni mama wa watoto wawili ambaye kuvunjika kwa ndoa yake kutokana na vituko vyake, kulimweka pabaya na akaanza kuonekana kama mtu wa ajabu. Hajaolewa tena mpaka sasa. Anaendelea kuponda raha.


                                                   

                                                     Faithia Balogun

Matukio yake ya kutwangana ngumi na wasanii wenzake ni mengi kuliko mazuri yaliyoripotiwa. Ameachana na mumewe, lakini bado anaendelea kutumia jina la ukoo wa mwanaume huyo na kulea watoto wake wawili.






                                                             

                                                           Stephanie Okereke
Alichapana makonde na Genevieve Nnaji mwaka jana kwa madai kwamba alikuwa akimmendea mumewe. Inadaiwa kuwa hajisikii vizuri Genevieve kuwa karibu kiutendaji na kiharakati na Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan. Hata hivyo Stephenie alibahatika kuolewa na Linus, haijulikani kama ndoa yao itadumu?
                                     
                                                                    

                                                          Mosun Filani
Alimng'oa mumewe kwenye uhusiano mwingine ambao ulikuwa na watoto wawili. Lakini wiki chache baada ya ndoa yake, mwanaume wake wa zamani akamuamuru amrudishie gari yake aliyokuwa amemnunulia na akairudisha kwa aibu.

 








No comments:

Post a Comment