Tuesday, January 6, 2015

Kauli ya waigizaji chipukizi hawauzi inamkera staa Lukuu


                                                                     
Hassan Lukuu
"Baadhi ya wasambazaji wa sinema  nchini,  wameibuka na  kituko kitakachosambaratisha soko la sinema za kibongo, kama  hawatakubali kuachana  na mawazo yao mgando ya kudai sinema bila ya msanii maarufu huwezi kuuza,"hayo yaliongewa na mwigizaji anayechipukia katika sanaa ya sinema Hasssan Lukuu.
Amesema  kabla ya kuwa na wasanii maarufu, watanzania walikuwa  wakinunua sinema na kuangalia sinema za waigizaji wasiowajua,  wapo waliokuwa wakinunua sinema za kihindi bila ya kuwafahamu waigizaji hao kama maarufu au sio maarufu.
Wapo waliokuwa wakinunua sinema za kichina, kijapan na kizungu. Baada ya kuingia sinema za kinaigeria watanzania walizinunua,  walipokuwa wananunua hawakujua kama waigizaji  hao ni maarufu, ila walinunua kwa ajili ya kupata burudani ya sinema.
Lukuu amesema  wakati kampuni ya Wananchi wote na kampuni ya GMC zilipokuwa zinasambaza sinema, hawakuwa na kauli za kutaka kusambaza kazi za waigizaji mastaa. Walikuwa wanasambaza kazi za  waigizaji wote wawe mastaa au chipukizi.
"Tukubali tusikubali kampuni ya wananchi wote na GMC zilichangia kuwepo kwa mastaa wengi wanaotamba leo,  bila ya kampuni hizo sidhani kama wangepatikana mastaa wanaokumbatiwa na kampuni mmoja inayojiona kama baba wa usambazaji na kufanya chochote wanachojisikia katika tasnia hii," alisema Lukuu.
Amesema kampuni hiyo haina lengo ya kunyanyua soko la sinema badala yake wanalengo la kuua soko,  ndiyo maana wanapokea na kuingia sokoni sinema zisizokuwa na ubora kwa sababu zimechezwa na mastaa.
Lukuu amesema wanachoangalia wao ni kupata fedha ya haraka haraka hata kama baadaye watu wasiponunua, wao watakuwa tayari wameshauza idadi ya kopi wanazotaka. Kwa staili hakuna soko la sinema litakalokuwa zaidi ya kuanguka na kupotea kabisa.
Kitu kingine kinachomboa na kumshangaza  kinachofanya na kampuni hiyo,  kuamini kama mwigizaji staa anauza wakati sio kweli. Kinachoouza ni unadishi mzuri wa script sambamba na uongozaji mzuri utakaofanywa na director.
Kama script ikiwa mbaya hata ukimchezesha Van Damme sinema itakuwa isiyoeleweka, imefika wakati watayarisha wa sinema wawatafute waandishi wa script wenye ili waandikiwe script zenye ubora wa hali ya juu. Mambo ya kubahatisha na kubabaisha yamepitwa na wakati.
Kwa upande waandishi wa script wanaovutia ni pamoja na Haji Dilunga na Ally Yakuti,  amedai waaandishi hao wanajua kuandika script zenye kukufanya ushindwe kunyanyuka kwenye mara unapoanza kuangalia sinema walizoandika.
Alitaja sinema ya Crazy Love iliyochezwa na marehemu Steve Kanumba, nyingine ni Morning Alarm aliyoshirikiana kuandika na Haji Dilunga. ilichezwa na marehemu Kanumba, Irene Paul  na Ben Branco.
Kwa upande wa Haji Dilunga amavutiwa na sinema ya Kwanini mama? Jamila na Pete ya Ajabu, Mwandishi pamoja na Bekitatu aliyoshiriki kucheza.
"Bekitatu inazungumzia maisha ya kweli ya kila siku yanayofanyika katika jamii yetu ya kitanzania, binafsi niliumizwa na baadhi ya scene za manyanyaso zilichezwa na Nuruti kumnyanya Hawa, nilijikuta nikitokwa na machozi ya kweli," alisema Lukuu.
Kwa mujibu wa maelezo yake alizaliwa miaka 26 iliyopita jijini Dar es Salaam,  elimu yake ya msingi na sekondari alisomea Boko,  akiwa shule alikuwa akijishughuliza uimbaji wa nyimbo  za bongo flave.
Wakati huo walianzisha kundi la muziki na wenzake linaloitwa Mako Mob,  walijaribu kuimba kwa muda mfupi na baadaye, aliachana na wenzake na kujiunga na kikundi kingine kinachoitwa LGL Brothers cha Makongo.
Kwa vile walikuwa hawana fedha za kuingia studio, alijiona kama vile anapoteza muda wake. Aliamua kujitumbukiza katika vikundi vya sanaa, miongoni mwa makundi alivyopitia ni pamoja na Uhuru Sanaa Group, Amkeni Sanaa Group, Navalonge Sanaa Group katika vikundi vyote hivyo alikuwa akifanya sanaa za ngoma na maigizo ya jukwaani.
Kwa vile alikuwa anataka kuigiza kwenye sinema aliamua kujiunga na kikundi cha Alwatan chenye maskani yake Ilala,  katika kikundi hicho alibahatika kucheza sinema mbili ambazo ni Julio na Romeo  na Sound of Soul.Wale wanaotaka nakala ya sinema yetu wasikose kupiga namba hizi 0753 833773 au 0655 833 772.

No comments:

Post a Comment