Friday, November 28, 2014
Waigizaji wa kiafrika, Kizungu na vimbwa
Waigizaji wengi wa Afrika wanapenda kuiga mambo ya Ulaya na Marekani. Kwa vile mastaa wengi wa Ulaya na Marekani wanapenda kutembea na vimbwa, hivi sasa kila anayejiona staa anatembea na kiumbe. Vipo vitu vya kuiga sio kutembea na viumbwa. Tuwe makini na mambo tunayoiga. Mastaa wengi wa Ulaya na Marekani wanatafuta vimbwa kwa ajili ya kujifurahisha kimapenzi, hayo yaliwekwa na mwandishi mmoja wa habari za kijamii nchini Marekani, Josephine Cris aliandika mtandaoni kuwa, mchezo huo uko sehemu nyingi ulimwenguni licha ya kwamba una madhara. “Mara nyingi wanawake wengi wanatumia mbwa kujifurahisha katika mapenzi, kwa sababu wanauwezo mkubwa kutumia ulimi kulamba kitu bila ya kuchoka. Wengi hufanya hivyo kwa siri kwani wanajua jamii itawashangaa kama watasikia taarifa zao. Ni vitendo vinavyochukiza sana hasa ukichukulia kwamba madhara ya kufanya mapenzi na mbwa yapo wazi. Hebu jiulize, kipi kinachoweza kukuvutia kwa mbwa hadi akupe mshawasha wa kufanya naye mapenzi, kwanza mnyama siku zote ni mchafu na anaweza kukuambukiza maradhi, sasa sijui kwa nini watu wanawatumia kimahaba,” anaeleza Josephine. Kwa upande wa waigizaji wa Afrika, hatujui kama wanahusika au ni kuiga bila ya kujua wanachoiga. Tuwe makini na vyakuiga sio kila kitu tunaiga.
Maajabu makubwa, binti amefunga ndoa na mbwa
.
Kufundoa na mbwa
Binti amefunga ndoa na mbwa kwa ajili ya kuondoa mikosi na majanga ya kimaisha, harusi hiyo imefanyika hadharani bila ya kuficho chochote. Wazazi wa mwanamke wafurahia kama vile binti yao ameolewa na mtoto wa tajiri namba moja duniani. Hebu niambie duniani inaelekea wapi? Tutafakari na kumrudia mungu wangu kwa kufanya ibada ya kweli na sio ibada za kinafiki. Hatuwezi kujua lini duniani itafika mwisho kama vitabu vya dini vinavyosema.
Kufundoa na mbwa
Binti amefunga ndoa na mbwa kwa ajili ya kuondoa mikosi na majanga ya kimaisha, harusi hiyo imefanyika hadharani bila ya kuficho chochote. Wazazi wa mwanamke wafurahia kama vile binti yao ameolewa na mtoto wa tajiri namba moja duniani. Hebu niambie duniani inaelekea wapi? Tutafakari na kumrudia mungu wangu kwa kufanya ibada ya kweli na sio ibada za kinafiki. Hatuwezi kujua lini duniani itafika mwisho kama vitabu vya dini vinavyosema.
Chike Ike akitesa Dubai kwa raha zake, Mambo ya fedha
Chike Ike kwenye boti
Chike Ike akiburudika na kahawa
Chike Ike akipata mchana mwema
wakiwa ndani bori
Chike akiwa kwenye fukwe
Chike akiwa kwe boti
Marehemu Marijani Rajabu aliyekuwa mwanamuzki wa Dar Intenatinal aliwahi kuimba pesa ni sabuni ya roho. Mwenye pesa akifika watu wote wanasimama kila analosema watu wanalipa uzito hata kama ni wazo la kijinga. Ndiyo ilivyokuwa kwa muigizaji wa Nigeria, Chika Ike akitumia fedha anavyotaka katika fukwe ya jiji Dubai ambapo unaambiwa alikodi boat kwa dola elfu 24,000 kwa muda wa siku mbili tu, na kila alilosema alisikilizwa na lilitekelezwa kwa kasi ya ajabu. PESA ni mfalme wa dunia, ukibisha wewe bisha lakini ndio ukweli wenyewe.
Thursday, October 30, 2014
Mwandishi yafichua machafu ya watu
Wapenzi wa kazi za Haji Dilunga, tarajieni kupata sinema nyingine ya Mwandishi wa habari. Script nimeandika katika ubora wa hali ya juu, Kama uliburudika na Kwanini Mama sambamba Jamila na Pete ya Ajabu. Mwandishi ni zaidi ya kile unachofikiria. Ni sinema aliyotumia muda mwingi kufanya utafiti wa namna ya fani ya habari inavyotumika kwa faida ya wajanja wachache. Ni ujanja gani? Na nani anafanya ujanja huo ni kuitafuta DVD ya sinema iliyoingia hivi karibuni. Imetayarisha na Kampuni ya Big One Entertainment. Daima ubora kwanza. Kama kawaida imeatungwa nakuandikwa na Haji Dilunga
Kwanini Mama yatoa wengi machozi
Kwanini mama ni sinema inayozungumzia maisha ya watoto wa kiume wanavyowanyanyasa mama zao na kuwasikiliza wake zao. ni sinema yenye mafunzo ya hali ya juu sio vizuri kuikosa. Stori na script ni kazi ya Haji Dilunga.
Jamila bado inatesa sokoni
Ile sinema ya Jamila na pete ya ajabu bado inaendelea kuvutia wengine,kila kukicha wapenzi na mashabiki wamekuwa wakiizungumzia. Ni sinema inayozungumzia unyanyasaji wa watoto. Imetungwa na Haji Dilunga.
Jamila akicheza na nyani
Jamila akicheza nyani
Jamila akipanda ngamia
Jamila akiwa juu ya ngamia
Jamila akicheza na nyani
Jamila akicheza nyani
Jamila akipanda ngamia
Jamila akiwa juu ya ngamia
Thursday, October 10, 2013
Sound of Soul itakuwa mitaani hivi karibuni
Sinema ni sanaa ya maigizo kwa njia ya vitendo, inayoelimisha jamii kwa mfumo wa picha. Lengo la mtayarishaji kutengeneza sinema ni kutaka kufikisha ujumbe kwa jamii iliyotuzunguka.
Wataalamu wa sanaa ya sinema, wamebainisha kwamba sinema imegawanyika katika makundi tofauti, kuna sinema zinazohusu maisha ya mtu fulani au famila. Sinema nyingine zinahusu jamii husika, mfano sinema ya Sound of Soul, inaelezea madhara ya tamaa katika jamii yetu ya kitanzania.
Kwa mujibu wa maelezo ya msemaji wa kampuni ya Swahili World Picture, Haji Dilunga
ambaye ndiye mtunzi na mwandishi wa script hiyo, amesema kisa hicho kiliwahi
kutokea miaka ya nyuma kabla ya yeye (Dilunga) hajazaliwa, baada ya kusimulia
aliamua kutayarisha sinema ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Dilunga ambaye ni mwandishi wa habari, amesema kisa hicho amekiboresha ili kiweze
kuwa na mvuto kwa watazamaji, pamoja na kuongeza matukio ya kusikitisha na
kuhuzunisha.
Amesema sinema hiyo inamzungumzia msichana Whitney, aliyekuwa na tamaa ya kutafuta
mali baada ya mali za urithi alizoachiwa na marehemu baba yake, kunyang'wa na Baba
yake mkubwa, alipokuwa na mdogo na hatimaye kufukuzwa kwenye nyumba yao pamoja na
mama yake.
Kitendo hicho kilimfanya Whitney kutafuta mali kwa udi na uvumba, ili aweze kuwa
na maisha mazuri. Kwa bahati nzuri alifanikiwa kuwa na maisha mazuri, baada ya
muda mfupi maisha mazuri yalimtumbukia nyongo.
Ni nani aliyesababisha maisha mazuri yamtumbukie nyonge, ni msichana mwingine
anayeitwa Lolita, Msichana huyu alitokea kumsumbua Whitney kupita kiasi. Nini
matokeo ya usumbufu wa Lolita kwa Whitney? Unajua kwanini alimsumbua? Jibu
utalipata baada ya kuangalia Sound of Soul.
Utamu wa sinema hiyo unakuja pale unapotaka kujua kama sio kufahamu, kilichompata
Baba yake mkubwa Whitney, baada ya kumnyang'anya mali Whitney. Alifanikiwa kutimia
mali hizo, au alizikimbia na kuchukuliwa na watu wengine? Ukibahatika kuangalia
Sound of Soul utafahamu kisa hicho cha kusisimua.
“Nadhani wale wanaofuatilia sinema ninazotengeneza, watakubaliana na mimi kwamba si bahatishi katika utunzi na uandishi wa script sambamba na kuidirect movie. Watakumbuka sinema zangu nilizoandika script na kudirect ni pamoja na Uwanja wa dhambi, I love you, Picnic, Bunge la Wachawi, Popobawa na Zindiko." Alisema Dilunga.
Sound of Soul inawataka vijana kutafuta mali au fedha kwa njia ya halali, pia wanatakiwa kufahamu kama umauti pia upo nyuma yetu. Kutafuta fedha au mali kwa njia zisizokubali na jamii yetu au muumba wetu, nikujitafutia matatizo katika maisha yako ya duniani na kesho ahera.
“Sisi ni tofauti na watengenezaji wengine wa sinema, sisi hatutengenezi sinema zenye visa vya mapenzi ya kufikirika. Tunatengeneza sinema zenye ujumbe wa visa vya kweli katika maisha ya binadamu." Alisema Dilunga.
Amesema Sinema kama uwanja wa dhambi ilivuma sana, mpaka leo bado watu wanaikumbuka. Kuna baadhi ya wapenzi wa sinema walitoka Mombasa kuja kuonana na waigizaji wa sinema ya uwanja wa dhambi.
“Hebu fikiri watu wamefunga safari toka Mombasa kuja Dar kuonana na waigizaji waliocheza uwanja wa dhambi, sio jambo la kawaida kutokea katika sanaa. Mara nyingi tumezoea kusikia na kuona watu wakitoka mikoani sio nje ya nchi." Alisema Dilunga.
Amesema Sound of Soul ni sinema nzuri inayofaa kuangalia na familia yako, kwa sababu imezingatia maadili ya kitanzania. Hakuna mwigizaji yoyote aliyevaa nguo za ajabu kama nusu uchi, unaweza kuangalia na watoto wako bila ya kujisikia vibaya.
Sinema hiyo imechezwa na Mwajuma Abdul Haji, aliyecheza kama Whitney. Fatuma Mwinchumu amecheza Mama Whitney, Jimmy Raphael amecheza kama Baba mkubwa. Nurati Ngereshi amecheza kama Lolita.
Wengine waliocheza majina ya kiuchezaji yakiwa kwenye mabano ni Zalka Athumani (Rose),Emilio John (Mganga Puchiro),Sikudhani Mkambo( Mke wa Puchiro), Clemencea Salum (Tina), Khadija Fundi(Bi Upupu), Peter Pascal (Mganga Chanuo),Apolinary Mathew(Bonzo) Abdullah Hassani (Bwino), Paul Leonard(Meneja), Amina Omary (Polisi), Paskazia Peter(Polisi), Halima(Magret),Yusuph (Polisi) na Said (Polisi)
Sound of Soul inatarajia kuingia sokoni mara baada ya kumalizika kueditiwa, kuna scene kama tatu zinafanyiwa marekebisho kwa ajili ya kuwapatia wapenzi uhondo wa aina yake.
Kwa wale vijana wanaotaka kuendeleza vipaji vyao, wanaweza kufika ukumbi wa CCM tawi la Amani siku ya jumanne, alhamisi na jumamosi saa kumi jioni. Au wanaweza kupiga simu namba 0789 904 226 au 0657 675 531.
Subscribe to:
Posts (Atom)

















