Showing posts with label Fedha. Show all posts
Showing posts with label Fedha. Show all posts
Friday, November 28, 2014
Chike Ike akitesa Dubai kwa raha zake, Mambo ya fedha
Chike Ike kwenye boti
Chike Ike akiburudika na kahawa
Chike Ike akipata mchana mwema
wakiwa ndani bori
Chike akiwa kwenye fukwe
Chike akiwa kwe boti
Marehemu Marijani Rajabu aliyekuwa mwanamuzki wa Dar Intenatinal aliwahi kuimba pesa ni sabuni ya roho. Mwenye pesa akifika watu wote wanasimama kila analosema watu wanalipa uzito hata kama ni wazo la kijinga. Ndiyo ilivyokuwa kwa muigizaji wa Nigeria, Chika Ike akitumia fedha anavyotaka katika fukwe ya jiji Dubai ambapo unaambiwa alikodi boat kwa dola elfu 24,000 kwa muda wa siku mbili tu, na kila alilosema alisikilizwa na lilitekelezwa kwa kasi ya ajabu. PESA ni mfalme wa dunia, ukibisha wewe bisha lakini ndio ukweli wenyewe.
Sunday, July 14, 2013
Sitaki wanaume wenye fedha- Jacqueline Wolper
Jacqueline Wolper
Mwigizaji wenye aliyeshinda tuzo ya mwanamke mwenye mvuto Jacqueline Wolper amesema hawapendi wanaume wenye fedha kwani wengi wao ni wanaume za wanawake wengine sio rahisi kuonyesha mapenzi yao ya dhati kwake, pia hawezi kutembea nao hadharani kwa kuhofia ndoa zao.
"Unajua unapokuwa na mwanaume mwenye fedha wakati ni mume wa mwanamke mwingine, hamtaweza kutembea pamoja, lakini ukiwa na kijana mwanzako hata kama hana fedha mtaweza kuongozana na kufurahia mapenzi wenu," alidai Diva huyo mwenye macho ya mvuto, sio kwa wanaume hata wanawake wenzake wametokea kumpenda.

Saturday, July 13, 2013
Lindsay mrembo mwenye matumizi mabaya fedha
Lindsay Lohan
Lindsay Lohan
New York, Marekani
Mwigizaji, Lindsay Lohan ni miongoni mwa warembo waliokuwa katika chati ya juu kwa kuvuta hisia za wengi kutokana na muonekana wake sambamba na vituko vyake, anavyofanya kila kukicha.
Mwanadada huyo anayependa kutumia fedha vibaya kama vile ameokoa, wakati ni fedha zake alizopata kwa kufanya kazi usiku na mchana. Jarida la Forbes la mwaka jana, limeandika kwamba Lindsay ameshika namba thalethini katika orodha ya waigizaji wanaotafuta fedha ili waweze kuishi maisha mazuri.
Lindsay mwenye umri wa miaka 27 raia wa Marekani ana utajiri wa dola 11 milioni.Utajiri huo umetokana na uigizaji, uimbaji wa muziki, uanamitindo na utangazaji wa manukato.
Kutokana na matumizi yake kuwa mabaya, mwaka 2011 alijikuta akifikia hatua ya kufilisika, mahesabu ya haraka aliyofikia ili aweze kupata fedha, ni kupiga picha za utupu na kupata dola milioni moja. Baada ya kupiga picha hizo alipata fedha na kurudi tena kwenye chati ya wenye fedha.
Kwa kutaka kuonyesha jeuri ya fedha alipangisha nyumba kwa dola 10,000 kwa mwezi. Anatumia dola 800 kila wiki kwa ajili ya kutengeneza nywele zake, alinunua gari aina porsche kwa dola 80,000.
Amekamatwa mara nyingi kuhusiana na utumiaji wa madawa ya kulevya na kuendesha gari akiwa amelewa, mwaka 2007 aliwahi kufungwa jela kwa muda wa siku tisini baada ya kupatikana na hatia ya kufanya fujo.Kutokana mwendo wa tabia zake kuwa tofauti na jamii iliyostarabika, Lindsay anapata ushauri wa kuacha kutumia dawa za kulevya.
Subscribe to:
Posts (Atom)