Tuesday, February 3, 2015

Maradhi ya kufanya manunuzi yawakumba wanawake


                                                                     
                                        Wanawake wakiwa dukani  na mifuko ya bidhaa zao
                                             Mwanamke akiwa dukani akijaribu viatu
                                             Mwanamke akiwa tayari amenunua bidhaa zake
                                       Mwanamke akiwa amechukua bidhaa zake anaondoka
                                          Mwanamke akiwa anajaribu viatu ili aweze kununua

Duniani kuna maradhi mengi sana yanayoibuka kila kikicha, hivi sasa dunia inasumbuliwa na maradhi ya kisaikolojia kuliko maradhi ya kimwili.  Hivi karibuni yamegundulika maradhi mapya  kwa wasichana na wanawake.  Maradhi hayo yanafahamika kama  shopping umegundulika aina mpya ya ugonjwa maarufu kwa wanawake wengi, Lakini hawajui yaani maradhi ya kupenda kufanya manunuzi ya nguo, viatu na mapambo. Chunguza kuanzia wasichana wa shule vyuo mpaka wamama wanao  maradhi hayo . Yaani mtu Ana nguo makabati chumba kizima viatu kibao Lakini bado anataka kuingia dukani anunue nguo mpya!  viatu vipya!  Watalaam wa maradhi ya akili wamesema shopping maradhi yanayoisumbua dunia kwa sasa, hasa kina dada na kinamama.. Tiba ya maradhi hayo ni ushauri zaidi kuliko vidonge au shindano.  Hata hivyo tafiti zinaonyesha hata baadhi ya wanaume wameanza kukumbwa na maradhi hayo, hasa wale wanaojifanya masharobaro.

No comments:

Post a Comment