Showing posts with label Obiekwe. Show all posts
Showing posts with label Obiekwe. Show all posts

Friday, February 6, 2015

Mazishi ya Muna Obiekwe, na kile usichojua kuhusu maisha yake

                                                         
                                                             Marehemu Muna Obiekwe
KIFO cha mwigizaji maarufu  wa Nollwood, Muna Obiekwe kimezua gumzo kwa wapenzi na mashabiki wake, sambamba na wale  wasiokuwa mashabiki wake ila wanafuatilia tasnia ya filamu nchini Nigeria,  kuna mambo kadhaa ambayo yawezekana ulikuwa huyajui kuhusu staa huyo aliyefariki kutokana na matatizo ya figo.
Wapo watu waliosema Muna alikuwa muoga wa waandishi wa habari hakuwa tayari kujitokeza hadharani, kuomba kuchangishiwa fedha kwa  ajili ya matibabu yake.  Kwa sababu hakupenda watu kujua maisha yake binafsi.
Wengi wanasema kwamba hakutaka kuchangisha  kwa kuhofia kujishusha kutokana na umaarufu aliokuwa nao, ingekuwa aibu kwa kwake.  kwa watu watajiuliza  atashindwa vipi kujitibia mpaka atafute fedha za michango, wakati wanapatiwa malipo mazuri.
Inaelezwa kwamba Muna alikuwa akinywa pombe sana, licha ya kukatazwa na daktari kunywa pombe. Alikuwa akijihudumia mwenyewe bila msaada wa watu wengine, lakini baadaye siku za mwisho za uhai wake alipata msaada mkubwa kutoka kwa mwanamama Patience Ozokwor na Kanayo O. Kanayo.                                                              
                                                Gari iliyobeba jeneza la Muna Obiekwe
Licha ya kuwa  mtu wa kuona aibu sana kueleza matatizo ya maisha binafsi,  siku za mwisho za uhai wake aliwasiliana na muigizaji wa kike wa Nollywood, Ibinabo Fiberesima lakini hakuwa na msaada kwa sababu  alifariki siku chache baadaye.
Alijua tatizo hilo siku nyingi lakini inaelezwa kuwa alijua atalitatua kimya kimya, aliyapuuzia maumivu aliyokuwa akiyasikia. Muna alikuwa na mke na watoto wawili lakini wengi hawakujua alikuwa akifanya maisha yake siri kubwa.                                                                    
                                          Baadhi ya waigizaji wa Nigeria wakiwa katika mazishi
Habari ziko nyingi sana Nigeria baada ya msanii huyu kupoteza maisha. Wamoja wanasema kwamba alikufa kwajili ya kuendeleza pombe kwa kiasi kama inavyoojulikana alivyokuwa anaitumia. Wengine wakasema kwamba alikufa na ugonjwa wenyewe wa kifafa baada ya yeye kusema kwamba alikuwa ameishapona.
Kama inavyojulikana  Muna ameacha pengo kubwa sana Nigeria kutokana na ujuzi wa uigizaji wake. Aliwahi kuigiza katika sinema  inayoitwa  Men in Love,  sinema iliyopigiwa kelele sana Nigeria wakidai itachangia kuhamasisha ushoga.
 Inasemekana kwamba aliweza kunywa pombe kwa kiasi kikubwa , ila director akisema action anaingia kwenye scene utazani ajalewa. Hiyo ni moja ya sifa yake tofauti na wengine wakilewa hawawezi kucheza vizuri. R.I.P Muna Obiekwe.

Sunday, February 1, 2015

MAZIKO YA MUNA OBIEKWE KUFANYIKA KESHO FEBRUARI 3, 201


                                                   Muna Obiekwe enzi za uhai wake

                         Moja ya sinema aliyoshiriki kucheza Muna Obiekwe

                                          Sinema nyingine aliyoshiriki kucheza Muna Obiekwe

                                             Kitu kingine alichosiriki  Muna Obiekwe


Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa chama cha waigizaji Nigeria (AGN), Ibinabo Fiberesima ametangaza ratiba kamili ya mazishi ya mwigizaji wa Nollywood, Muna Obiekwe.  Mwigizaji huyo alifariki dunia Januari 18, 2015 baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo ambayo alikuwa ameyafanya siri kwa muda mrefu. Ibinabo Fiberesima amesema maziko ya Muna yanatarajia kufanyika  kesho,  Februari 3, mwaka huu katika eneo la Umudioka, Jimbo la Anambra nchini Nigeria.  wapenzi na mashabiki sambamba na waigizaji wnzake watakutana  Marsha eneo la makutano ya Surulere kisha kuelekea Uwanja wa Ojez. Mavazi yatakuwa ni tisheti nyeupe ambazo zitatolewa eneo hilo.