Tuesday, September 27, 2016

MWAJUMA AU MAIMUNA amefariki dunia


Huwezi kuamini lakini ndio hivyo imetokea, jumapili ya tarehe 28 mwezi wa nane, ni siku tuliyompoteza msanii mkongwe Mwajuma Abdul maarufu kwa jina la MAIMUNA. Akazikwa jumatatu tarehe 29 saa kumi katika makaburi ya kisarawe. kwa wale wanaofuatilia matangazo ya redio watamkumbuka kwa tangazo la HII SASA SIFAAA, NA LEO TENA NYAMAAA, ni miongoni mwa matangazo kati ya mengi aliyocheza. Katika televisheni anakumbukwa kwa matangazo mengi aliyofanya ila kwa haraka tangazo la kifua kikuu akiwa na Kaboba, Onyango na wengine. Baadhi watamkumbuka kwa michezo ya redio, hasa mchezo wa TWENDE NA WAKATI uliokuwa ukirushwa na redio Tanzania kwa sasa TBC. Kwa upande wa sinema ameshiriki sinema nyingi baadhi Ni UWANJA WA DHAMBI. Jina la MAIMUNA alilipata baada ya kushirikia katika sinema ya UWANJA WA DHAMBI, sinema iliyompatia umaarufu mkubwa. Baadhi ya sinema alizoshiriki ni pamoja na I LOVE YOU, LAZIMA UFE JORAM, PICNIC, BUNGE LA WACHAWI, POPOBAWA, ZINDIKO, BOSS nk. Pia aliwahi kushiriki tamthilia ya HUKUMU YA TUNU akitumia jina la TUNDA. Amefariki akiwa tayari amecheza sinema inayoendelea kueditiwa pamoja na Tamthilia inayoendelea kueditiwa. Amefariki ghafla hakuwa na maradhi yoyote, alikuwa mzima wa afya njema. Mpaka saa mbili usiku alikuwa mzima wa afya katika sherehe ya kitchen part ya ndugu yake, Ghafla alijisikia kuishiwa na nguvu na kuanza kutapika, hali hiyo iliendelea mpaka alivyokimbizwa Amani Hospital, hatimaye akafariki dunia muda mfupi.Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un