Sunday, March 1, 2015

Viatu vya kishetani, ukivaa unamsambaza kwa nguvu moja.


          

               
Ukivaa unaendelea kumtukuza na kumsambaza shetani kwa wengi,    sio kila kinachotengenezwa na wabunifu ni  lazima ukivae.  Vitu vingine vinatengenezwa kwa sababu maalumu, watengenezaji wanajua wanachofanya, hakuna anayebahatisha katika hilo. Miongoni mwa wabunifu na watengenezaji wa mitindo mbali mbali ni wafuasi wa dini ya shetani. Kuweni makini katika kuchagua aina gani ya kiatu unachotaka kuvaa. Hasa kina dada wanaongoza kwa kuwa na mitindo mingi ya viatu na nguo.  Kwa vile wabunifu wanajua kama waigizaji, wanamuziki na wanamitindo wa mavazi ni watu wanaotazamwa sana na jamii, wanawavisha viatu hivyo kwa lengo la kuvitafutia soko na umaarufu miongoni mwa jamii ili shetani aweze kuwa na nguvu. Hivi sasa viatu hivyo vimeanza kutumika sana katika sinema mbali mbali au katika baadhi ya video za wanamuziki maarufu. Wakati mwingine vimekuwa vikitumika katika majukwaa ya wanamitindo. lengo ni kusambaza nguvu za shetani. kuwa makini kama unapenda kuigi kila kitu.

Mwanamume ametumia pauni 150,000 kutaka kufanana na Kim Kardashian


                                                                           
                                                                     Jordan James

                                                                   Kim Kardashian                                                                     
                                                                   Jordan  na Kim                                                                    
                                                                         Jordan                                     


                                                               Jordan akiwa na mkoba

                                                                  Kim akiwa mkoba
Kutana na kijana Jordan James kutoka Uingereza mwenye umri wa miaka 23 ambaye ari yake maishani ni kufanana tu kama Kim Kardashian.Mvulana huyu amefanya mambo ya ajabu akijitahidi kufanana na Kim kwa kujiongeza urembo bandia, hasa kufanya midomo yake kuwa mikubwa akitaka ifanane na ya Kim.
Je unajua ametumia kiwango gani cha pesa katika harakati zake za kutaka kufanana kama Kim? Pauni 150,000 au dola laki mbili na arobaini.
Pesa hizo zote amezitumia kwa kufanyiwa upasuaji na kuongezwa urembo bandia. Cha kushangaza ni kwamba huyu ni mwanamume anayetaka kufanana kama mwanamke
Jordan James hutumia mamia ya dola kujiweka urembo bandia na kufanana na  kichekesho kwa wengi. Amekua akitazama mamia ya picha za Kim akipiga pozi kumuiga
Aliambia jarida la The Sun kwamba alianza kumuenzi Kim Kardashian mwenye umri wa miaka 33 baada ya kutazama makala ya kipindi kijulikanacho kama ''Keeping Up With The Kardashians.'' Kipindi kinachohusu Kim na Familia yake.
'ninapenda kila kitu kumhusu Kim,' aliambia The Sun. 'yeye ndiye mwanamke mrembo zaidi duniani. Ngozi yake ni nyororo, nywele zake zinapendeza yaani kila kitu kumhusu kinanipendeza. ''
Jordan amefanyiwa upasuaji kuongeza urembo bandia zaidi ya mara 50 katika juhudi zake za kutaka kufanana kama Kim, amerembeshwa midomo, ametolewa nywele kwa kutumia miale ya Laser , amewekwa Tatoo na hata kubadilisha kope zake na mengine mengi.
Lakini mabadiliko haya yote yamemgeuza sura sana Jordan na kumanya kuwa kichekesho kwa watu wengi.
''Mimi mwenyewe hucheka watu wanapojaribu kunitusi au kunikejeli, na kuniambia kwamba mimi ni kama tu plastiki, yaani kila kitu mwilini mwangu ni baandia. Lakini hio hainijalishi.'' alisema Jordan kwa mapozi yote ya kike aliyoiga toka Kim.